Niionavyo Tanzania miezi michache ijayo

Niionavyo Tanzania miezi michache ijayo

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,198
Reaction score
162,742
Uchaguzi mkuu wa mwaka huu, endapo utafanyika, hautaicha Tanzania ikiwa salama na mwaka huu ndio Tanzania itajulikana zaidi kimataifa(ita-make the headlines).

Kumbuka,nchi za kiafrika hutangazwa sana duniani na vyombo vya habari vya kimataifa si kwa mazuri,bali tu pale panapokuwa na machafuko au ghasia za kisiasa na magonjwa kama vile Ebola n.k.Tanzania mwaka huu sidhani kama tutalikwepa hili.

Mwaka huu kuna kila dalili na kila sababu ya wapinzani(UKAWA) kususia au kupinga matokeo ya uchaguzi huu na hivyo kusababisha sintofahamu kubwa katika nchi hii.Sababu hizo ni kama ifuatavyo;

Mosi,zoezi la kuandikisha wapiga kura linafanyika katika mazingira yasiyo rafiki kwa wapiga kura na hali hii huenda ikasababisha wananchi wengi wakashindwa kujiandikisha na baadae kuzua malalamiko na hivyo kuufanya uchaguzi ujao usiwe huru na wa haki.

Kwa mfano,jana kupitia ITV,nilishuhudia wananchi wakilalamikia zoezi la uandikishaji huko Iringa kwamba linachukua muda mrefu na kuwafanya wengine wafike kwenye vituo saa 8 za usiku ili kuwahi kuandikishwa na dada mmoja alifika mbali zaidi kwa kusema zoezi hilo linahatarisha ndoa zao kwani hutumia muda mwingi kukaa vituoni kuanzia saa 12 za asubuhi.

Mbali na wananchi, hata viongozi wa vyama vya siasa nao wameulalamikia mfumo huu mpya wa uandikisha wapiga kura unaojulikana kama BVR bila kusikilizwa licha ya ushauri mzuri wanaoutoa kwa viongozi wa nchi hii.

Pili, vijana wengi hawataipigia kura CCM na hivyo kuifanya CCM kushindwa vibaya na ni vijana hao hao ndio baadhi yao watakosa fursa ya kujiandikisha kutoka na mfumo huu wa BVR na wengi wao hawatakubali kupoteza haki hiyo.

Tatu,kashifa za Escrow,unyama wa polisi,maslahi duni ya wafanyakazi na hasira ya wafanyabiashara kwa serikali zitakipunguzi CCM kura nyingi na kuongeza uwezekano wa CCM kushindwa.

Nne,muungano wa UKAWA safari hii utawafanya wapinzani wawe wenye nguvu zaidi katika kudai haki yao na pia unaweza ukawafanya wakatae hata ku-compromise kwani teyari wana umoja na isitoshe mawazo na maoni yao mengi yamepuuzwa na watawala kiasi cha kutosha.

Kitakachotokea ni CCM kujaribu kuchakachua matokeo na kulazimisha ushindi na hapa UKAWA hawatakubali na ndio itakuwa mwanzo wa vurugu na machafuko nchi nzima.

Katika majimbo mengi,wabunge wa chama tawala watashindwa ila tume haitatoa matokeo kwa wakati na wananchi kwa kushirikiana na wabunge walioshinda hawatavumilia na machafuko yatatokea sehemu nyingi za nchi kwa wakati mmoja na polisi watashindwa kutuliza hizo ghasia na itakuwa ni fujo kila mahali(kwenye kila jimbo).

Matokeo ya uraisi yatakayotangazwa na tume,wapinzani hawatayakubali(kumbuka walitaka tume huru) na hivyo kuongeza hasira za wananchi na za viongozi wa upinzani.

Matokeo ya ujumla ya haya yote itakuwa ni fujo,ghasia na wapinzani kuhamasisha maandamo ya nchi nzima kupinga matokeo ya uchaguzi huo na kutaka uchaguzi urudiwe na safari hii usimamiwe na tume huru.

Viongozi wengi wa upinzani ikiwemo wagombea ubunge watakamatwa,watapigwa na kutiwa ndani kwa kitakachoitwa kuchochea vurugu na hapo ndipo vyombo vya habari vya kimataifa vitakapoimulika Tanzania na zaidi pale watu watakapopigwa, kujeruhiwa na hata kuuwawa katika ghasia hizo.

Wafuasi wengi wa upinzani na hasa vijana, hawatavumilia kuona Mbowe,Dr.Slaa,Mbatia na Lipumba wakipigwa virungu na polisi au kuona wabunge na madiwani waliowachagua wakikamatwa bila sababu za msingi.

Watawala,muda wa kufanya marekebisho na kuepusha balaa hili bado upo, ila kama mnataka kulazimisha ushindi,basi mjiandae kuhudhuria mahakama za kimataifa kama wenzenu wa Kenya.

Amani na utulivu wa nchii baada ya uchaguzi wa Oktoba iko mikononi mwa viongozi wa UKAWA na kamwe si polisi wala watawala.
 
Hapo ndipo nchi za zinazotaka gesi zitatumia fursa hiyo kujipenyeza
 
Huu uzi utafufuka baada ya miez kama 9 ijayo..sidhan kama hata network za simu kama zitakuwa hewan bt tutakutana Jf anyway...Umeongea mkuu.ni ukwel ambao wanafki tuu ndo watakuja kuupinga..
 
Hapo ndipo nchi za zinazotaka gesi zitatumia fursa hiyo kujipenyeza
Hilo linawezekana lakini sababu kuwa itakuwa ni kiburi cha watawala na si watu kutoka nje ya nchi.
 
Siyo kwamba ninataka kukupinga lakini naomba nikupe picha....Watanzania watajikuta wapo pamoja na nia yao ni mmoja ila baadhi ya wanaodhani wananguvu watakujakutambua hizo nguvu zimewatoka na zipo kwa watanzania...... Hao wachache watageukiana wao kwa wao wakidhani wamehujumiana na mwisho wa siku kila mmoja atajikuta ameingia kwenye mtego ambao hawezi kuchomoka zaidi ya kuwajibishwa hapo vumbi la uchaguzi litakapokuwa limetulia......

Mtanzania atakaye mwaga damu yake ni yule atakayejipeleka kwa wale anaodhani wana nguvu vinginevyo hakuna kitakachomuumiza mtu yeyote innocent....

Says the architecture of the mageuzi Tz in the mighty name of Jesus Christ of Nazareth.....

Kuna wakati niliwaambia hakuna mtu wakuzuia haya mageuzi na lazima tu uproot the rotten system ili tujenge upya!

Haijawahi tokea wala hakuna awezayekufumbua fumbo hili hata actors hawajui wanapokea command na coordination toka wapi.....Hii ndiyo nguvu tunayojivunia and thats why we are called Kings for the King is not if his words cannot rule!
 
Sijui kama nitakuwa nimekuelewa vizuri.

Unajua sometimes hata mimi huwa nakata tamaa na kupatikana kwa mageuzi katika nchi hii ila kitu ambacho naanza kukiona ni kuwa,watanzania wamekosa mtu wa kuwahamasisha na kuwaongoza katika kudai mabadikiko wanayoyataka.

Hata hivyo,sasa hivi naona upo uwezekano wa viongozi wa UKAWA kusimama kidete na kuongoza vijana kudai mabadiliko.

Naamini,viongozi wa UKAWA na makundi mengine katika jamii,wakishirikiana na kuwaongoza vijana kudai mabadiliko,civil disobidience is innevitable.

Wanachokosa vijana wa nchi hii leo hii ni viongozi wa kuwaongoza na kuwahamasisha kudai mabadiliko.

Viongozi wa UkAWA(waliopuuzwa) wakisimama kidete,vijana wa nchi kamwe hawawezi kuwaangusha.

Kwa maneno machache,hatima na amani ya nchi hii itaamuliwa na viongozi wa UKAWA na kamwe si polisi wala watawala.
 
Sijui kama nitakuwa nimekuelewa vizuri.

Unajua sometimes hata mimi huwa nakata tamaa na kupatikana kwa mageuzi katika nchi hii ila kitu ambacho naanza kukiona ni kuwa,watanzania wamekosa mtu wa kuwahamasisha na kuwaongoza katika kudai mabadikiko wanayoyataka.

Hata hivyo,sasa hivi naona upo uwezekano wa viongozi wa UKAWA kusimama kidete na kuongoza vijana kudai mabadiliko.

Naamini,viongozi wa UKAWA na makundi mengine katika jamii,wakishirikiana na kuwaongoza vijana kudai mabadiliko,civil disobidience is innevitable.

Wanachokosa vijana wa nchi hii ni viongozi wa kuwaongoza na kuwahamasisha kudai mabadiliko.

Viongozi wa UkAWA(waliopuuzwa) wakisimama kidete,vijana wa nchi kamawe hawawezi kuwaangusha.

Kwa maneno machache,hatima na amani ya nchi hii itaamuliwa na viongozi wa UKAWA na kamwe si polisi wala watawala.

Huo mshikamano ama hamasa ya vijana unatengenezwa na kuratibiwa hicho ndicho nacho maanisha.....

Its now very early for you to see and difficult to perceive ila as it will show up thats when you will recall.....its another level, just wait and see!
 
Mi nashauri tuendelee kuiombea nchi iwe na amani, tuombee wezi wa mali ya umma wakamatwe na waadhibiwe na kufilisiwa, tuombee Polisi wajitambue, tuombee tume ifanye kazi ya busara ili utulivu uendelee hata kama amani haipo
 
Mwaka huu CCM wataona rangi za kila aina. CCM wamechokwa, hakuna watakapo pona.

Vijana wamehamasika vya kutosha, picha tulianza kuipata serikali za mitaa, uchaguzi mkuu ndo unakuja.
 
Na ndipo ule mwisho utakapokuja mwenye sikio na asikie neno hili ambalo mleta uzi analitabiri....
 
Nawaza uchaguzi kufanyika bila tume huru ya Uchaguzi. Naona tabu> Nivema kudai tume hiyo kabla ya uchaguzi kuliko kuingia katika uchaguzi huku tume ikiwa ile isiyo huru!
 
Back
Top Bottom