NIGERIA: Rais Muhammadu Buhari arejea London kwa matibabu

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amerejea London kupokea matibabu wiki chache baada yake kukaa huko kwa miezi miwili.

Taarifa kutoka kwa ikulu ya rais huyo imesema amehitajika kwenda Uingereza kuchunguzwa na madaktari.

Hata hivyo, kufikia sasa hakuna taarifa kuhusu ugonjwa anaougua wala muda ambao anatarajiwa kukaa nchini Uingereza.

Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo anasema Jumapili ilikuwa siku muhimu kwa Muhammadu Buhari ambapo alikuwa anakutana na wasichana 82 wa Chibok ambao walikuwa wameachiwa huru baada ya kuzuiliwa na wanamgambo wa Boko Haram kwa miaka mitatu.

Badala yake, kutokana na afya yake, tukio hilo la kuwapokea halikufanywa kuwa sherehe kubwa.

Buhari amekuwa haonekani sana hadharani kipindi kirefu cha mwaka huu. Alikaa wiki saba Uingereza kabla ya kurejea Machi.

Wiki iliyopita, hakuhudhuria mikutano mitatu ya baraza la mawaziri huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu hali yake.

Alijitokeza hata hivyo Ijumaa wakati wa swala ya Ijumaa katika msikiti ulio ikulu ya nchi hiyo.

Taarifa kutoka ikulu imesema kiongozi huyo alikuwa amepangiwa kuondoka mapema Jumapili alasiri lakini akachelewa kwa muda kumuwezesha kukutana na wasichana hao wa Chibok.

Rais Buhari amesema: "Nina imani kwamba serikali itaendelea kutekeleza shughuli zake vyema nitakapokuwa nje ya nchi."

Chanzo: BBC Swahili
 
Hapa nahisi kuna kitu kinaendelea zidi ya Marais Waislamu wa Nigeria maana hata Umar Y'aradua yalikuwa hivi hivi.
 
Huyo ana dalili za mauti, inabidi aokoke haraka aachane na huo msikiti
 
Mungu Amponye. Ya Aradua (spelling?) naye alianza hivi hivi wakaficha kumbe keshafariki. Afadhali mwanaume Abacha alisizi baada ya ku-overdoze viagra huku amezungukwa na makahaba wa kimataifa kutoka India...
 
Hapa nahisi kuna kitu kinaendelea zidi ya Marais Waislamu wa Nigeria maana hata Umar Y'aradua yalikuwa hivi hivi.
Muhammadu Buhari ana miaka 74, Yaradua alifariki akiwa na miaka 58. Unaweza kuona mtu akishakuwa na umri mkubwa afya yake ni rahisi kuzorota na mara nyingi siku za kuwepo Duniani zinakuwa zimepungua... Acha hizo conspiracy theories zako mkuuu...
 
Duh, hii nchi na Zambia mbona zinakuwa hivi!
Lakini inatupa funzo kama binadamu kuwa afya zetu ziko mikononi mwa Muumba na hata huyo Shekau kajua haya labda ndio maana kaamua kuwaachia huru wale mabinti! Tumuombee apone haraka na kurejea kwenye majukumu yake.
 
Buhari akamuombe msamaha Jammeh

Chezea yahya junkung jammeh wewe ,

8cacda67f5438e4aa13a39a568566965.jpg
 
Back
Top Bottom