Wadau naomba mnisaidie.Mwezi wa sita mwaka huu nilimaliza kidato cha sita kisha nikapangiwa kwenda jkt kwa mujibu wa sheria.Nikiwa huko nilikutana na binti kutoka Iringa ambaye nilimpenda sana ila sikumwambia kwa kua kule jkt unaweza ukapewa adhabu mbele ya watu wengi hivyo sikuitaji mpenzi ili niwe huru kwaiyo mimi na binti yule tuliishia kuwa marafiki wa kawaida.Maisha yaliendelea pale kambini binti yule alikuwa ananisaidia kwenye shida ndogo ndogo na mimi pia nilimsaidia.Ilipofika siku ya kuondoka nilimtafuta sikumuona nikaamua niondoke zangu ila nikiwa nje ya geti gafla binti yule nilimuona akitoka ndani akafika eneo nililopo na akaniambia kwaheri akapanda piki piki faster na kuondoka sikupata hata muda wa kumuomba namba.Baada y hapo nilirudi nyumban dar ila nikiwa dar nilipewa namba ya rafiki yake wa karibu na mtu flani.Nilimuomba rafiki wa binti huyo anitumie namba ya binti huyo na akanitumia.Kipindi hiko post za chuo zilikuwa zimetoka na mimi nilikuwa nimechaguliwa chuo kikubwa Tanzania nzima kilichopo mkoani dodoma.Nilipo muuliza binti chuo alichochaguliwa na yeye alichaguliwa hapo ila coz tofauti na yang ila rafiki yake alichaguliwa hapo koz moja na mimi.Siku ya siku nilienda kuripot chuoni kabla yake yeye na rafiki yake.Baada ya mda mfupi na yeye alilipoti ila alifikia mjini kwa ndugu zake kwa kua hakukamilisha usajili ila badae akafika chuoni.Kuna siku nilimuomba tuonane akaniambia niende kwenye hostel zao na ni mbali kutoka nilipo ingawa chuo ni kimoja ila college tofaut umbali wake ni kama buguruni na mnazi mmoja mana chuo hiki ni kikubwa dodoma na Tz nzima.Nilipofika kule alikuwa apokei simu niliporudi nikamtumia sms ya kumlaumu na nikamwambia siongei nae tena akaniomba msamaha na nikamsamehe.Kesho yake nikaenda tena nikiwa nimependeza nilipofika nikaenda hadi hostel kwao hadi chumba chake alikuwa peke yake.Alinikaribisha kiti na yeye akakaa kitandan.Alinisifia nimependeza pia akasema anamatatizo mana amekuta vitu vya ajabu kwenye diary ya boyfriend mimi nikamtongoza akawa anakataa na akaniambia mimi ni handsome hataki presha mana mabinti wengi watanipenda mwisho akasema atanijibu.Nilimtafuta usiku akasema haiwezekani na kesho yake akaniambia anaye boyfriend.Nikamuuliza inamana mimi hunipendi akasema ananipenda sana ila hawezi kumiliki watu wawili nikimsumbua sana anaacha kuchat ndugu zangu nifanye nini huyu binti nampenda sana silali kwa raha kwajili yake.