1. Niki Mbishi alisema ameacha mziki
2. Wenyewe wana msemo wao "Hip hop ya kweli haipo redioni" , so wasiwalaumu watu wa media wasipopiga nyimbo zao coz wakizipiga itaonekana sio hip hop ya kweli (hiyo ni kwa mujibu wa msemo wao)
3. Jamaa wanafanya Hip hop ngumu sana, kuanzia beat hadi mashairi, Nikki akitaka nyimbo zake zichezwe afanye kama alivyofanya kwenye 'playboy' Mbona ulibamba sana, wakiendelea kufanya ngumu wataendelea kutusikilizisha masela tu geto kama Mimi hapa, nawakubali sana na nawasifia sana but hizi sifa nazowapa kwenye social network haziwafikishi popote. Tatizo letu masela ndo hivyo tunajua kusifia sana but CD zao hatununui, tunataka kupakua bure mtandaoni, hata kwenye show zao hatuendi. Kilingeni enzi zile ukienda unakuta mashabiki wako 30, tena kwa kiingilio cha buku jero, sasa hapa msanii anapata nini?
4. Hip hop ngumu kupata nafasi redioni ni tatizo, sio radio friendly. Na hili tatizo sio bongo tu hata unyamwezini ulikoanzia huu mziki, wanaotawala redioni/kwenye TV ndo hao kina Lil Wayne,Drake,Minaj,Young Thugs,etc wanaoimba kuhusu (f*ck,nigga,p*ssy,ass)
5. Ili ufikiriwe kuingia kwenye tuzo lazima nyimbo zako ziwe zinachezwa kwenye redios & tv, mashabiki wawe wanakufahamu, so sio kosa LA waandaaji tuzo, wenyewe wanaangalia ni wasanii gani wanatrend kwenye medias. Kuna kipindi nilikuwa Bukoba msimu wa pasaka, nilihudhuria kwenye mashindano fulan ya kuimba na kucheza yaliyokuwa yanafanyika beach. Sikuhiyo Songa aliambatana na wasanii wengine (hawana majina) kufanya show kwenye ukumbi maarufu unaitwa linas, sasa walikuja huko beach kupromoti show yao ya usiku maana kulikuwa na watu nyomi sikuhiyo aisee nilishikwa na huruma RAIA hawamjui kabisa Songa, MC alisema 'wangapi wanamjua Songa wanyooshe mkono, ilionekana mikono kama sita tu ukijumlisha na wakwangu, hili ni tatizo.
6. Wasanii hawa wanaofanya ngumu hasa wa Tamaduni hawako karibu na wadau wa media. Wanawatukana kwenye nyimbo zao/social network, usitegemee mtu unayemtukana apige nyimbo zako, mfano huyu wa kuitwa Nash MC anawatukanaga vya kutosha huko fb.
7. Media Redio/tv zinafanya biashara, hawawezi kupoteza mda wao kupromote kitu kinachopendwa na wachache, inaeleweka Hip hop ngumu zinapendwa na sisi 'masela', kundi kubwa ambalo ni (wazee,watu wazima,mabitoz, masista duu, watoto) ni ngumu kuwakuta wanasikiliza nyimbo dizain hiyo ya kina Nikki Mbishi, kama ni rap redio zitapiga hiphop laini za kina Bonge La Nyau coz hata masista duu wanaweza kusikiliza. Fid Q aliwahi kuanzisha kipindi chake kinaitwa 'FidFreestyle Friday' kinachohusu mambo ya Hip hop ila kilikufa kutokana na kukosa wadhamini, hii inadhihirisha kwamba Hip hop ngumu sio nzuri kibiashara
8. Nitaendelea....