mandella
JF-Expert Member
- Oct 29, 2011
- 3,051
- 3,255
Msemo unasema "age is nothing but number" Unaweza usiwe sahihi linapofika swala la Uongozi na Madaraka makubwa katika nchi. Niliwahi kuhisi Miaka 40, iliyowekwa kikatiba kumruhusu mtu kupata Fursa ya kugombea Uraisi wa nchi huenda ulikua si sahihi, ila kwa sasa nimegundua walioweka walikua na tafiti ya kutosha juu ya Swala hilo na zaidi walikua na umri sahihi kwa maamuzi ya jambo sahihi. Na ndio maana hata sasa pakitokea ukusanyaji wa maoni ya katiba mpya, nitabadili msimamo wangu, kwani nilipendekeza iwe chini ya miaka 40, na kwa sasa nitahitaji nafasi hii nyeti apewe mtu mwenye miaka 40 kuendelea kama katiba ya sasa inavyosema.
Mifano;..
1.Mnamfahamu Kim Jong_un , huyu ni kiongozii wa North Korea, alipata madaraka makubwa akiwa na umri mdogo, tazama matendo yake na maamuzi yake katika maswala ya nyeti katika nchi anayoiongoza.
2.Je , mnakumbuka Joto lilokuwepo kwa wana CCM pale Dodoma wakati wa Kumtafuta Mgombea Urais wa Tanzania, ni watu Gani waliotoka na Maamuzi sahihi ? Joto lile lilipoa ghafla. Nadhami mtakua mnaikumbuka Hiyo timu iliyoingia Chemba na Kutoka baada ya mda mchache.
3.Wote tunamjua Zitto Kabwe toka anazianza Siasa akiwa kijana mdogo, sasa jaribu kutofautisha Matendo ya ZZK alipozianza Siasa na sasa akiwa na umri wa miaka 40 ,Utakubalina na mm kwamba kwa sasa busara na Hekima zake zimeongezeka Mara Dufu.
4. Jaribu kuirudisha akili yako nyuma, Shule ya Msingi uliposoma na utafakari ni mtu wa namna Gani aliyekua anapata nafasi ya kua Kiranja mkuu(HP), thathmini pia ni Mtu wa umri gani alipewa nafsi ya kua Kiongozi wa Darasa. Nadhani mifano mingi mnayo hata katika ngazi za uongozi wa kifamilia na koo.
Mifano hiyo inanipeleka kuwaza kabisa kwamba umri, husaidia katika ukomavu wa kifikra huleta hekima katika kumsaidia kiongozi kufanya maamuzi.
Sasa Leo tumeona Kamishna mpya wa Kupambana na Madawa ya Kulevya amenza Kazi Rasmi, binafsi imenipa mwanga zaidi ya jinsi Umri Unavyotofautina katika kufanya "Apporoach ya Jambo" ikiwa ni pamoja na kulitafutia Suluhu sahihi Jambo Husika.
Jambo linaloonekana Zito sana na linaloogopesha na ambalo huwenda unakaza si sahihi kufanywa, hubadilishwa ndani ya sekunde moja na kuonekana ni jambo Jepesi na ni sahihi kufanyika.
Sitaki kuzungumza mengi Juu ya hili, zaidi iwe chachu na fundisho kwa vijana katika kujifunza siasa na uongozi Bora. Kiongozi bora hutanguliza hekima, busara, na utulivu wa akili mbele katika kutatua tatizo fulani na si kulichokua jambo hilo kihisia zaidi.
Binafsi naingunga vita ya Madwa ya Kulevya 100% na Italeta matokeo chanya Emdapo tu , .......
1.Operation itapata mkakati madhubuti na intellegencia inayotumia akili kubwa , maarifa na Busara ya juu kuliko kuinvest akili nyingi katika kufanya jambo hili Physically.
2.Jamii ikashirikiana kikamilifu na Idara husika zilizojitoa kwa dhati kupambana na Janga hili.
Ni Hekima na busara pekee ndivyo vitakavyofanikiksha Vita hii bila kuacha mtafaruku wowote kati nchi baina ya Vyombo vya Usalama Vs Jamii, Jamii Vs Viongozi , wala Mtu Vs Mtu. Na badala yake Tutaiokomboa Tazania yetu katika Vita hii ya Madawa ya Kulevya effectively pasipo kuzalisha na kuacha vita nyingine ya Kijamii.
Tanzania Bila Madawa ya Kulevya Inawezekana.