niameamua kusimama upande wa ukawa

niameamua kusimama upande wa ukawa

hard core

Member
Joined
Jan 11, 2015
Posts
46
Reaction score
28
NIMEAMUA KUSIMAMA UPANDE WA UKAWA NA KUMPIGIA KURA LOWASA AWE RAISI KWA MOYO MWEUPEE!!

Baada ya kutafakari kwa kina, Na kwa muda mrefu sana.... Nimeamua Kumpigia kura edwardlowassa kuwa Rais wangu wa awamu ya tano wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania bila kujali kashfa zake. Kama kweli alikuwa ana hatia, hao wanaohubiri kashfa hizi ndio waliotakiwa kumfikisha mahakamani.

Nimeamua kwa Moyo mweupe, Akili Timamu, Bila kushawishiwa na kwa uthabiti kumpigia Lowassa kura kwasababu zifuatazo; - Hatia yake ingethibitishwa na Mahakama pekee.
-Wanaomtuhumu leo (CCM) na serikali walitakiwa kumfikisha mahakamani.
.
-Chini ya CCM wanafunzi wanakaa chini

-Chini ya CCM huduma ya Maji ni shida

-Chini ya CCM rushwa na ufisadi umekita mizizi.

-Chini ya CCM shilingi imeporomoka na kufariki.

-Chini ya CCM huduma ya Afya ni shida

-Chini ya CCM Wajawazito wanajifungulia chini mahosptalini

-Chini ya CCM gharama za maisha zimepanda kukithiri.

-Chini ya CCM ajira hakuna kwa wasomi.

-Chini ya CCM viwanda vimekufa

-Chini ya CCM mashirika ya Umma yamekufa.

-Chini ya CCM Rasilimali zinatumika hovyo.

-Chini ya CCM Twiga wamepanda ndege bila kuonekana na rada.
Hawa twiga sijui walikuwa na Passport!

-Chini ya CCM waandishi wa habari wameuawa.

-Chini ya CCM maelfu ya wanavyuo hawana mikopo

-Chini ya CCM Elimu ya kuanzia shule ya Msingi hadi Chuo kikuu imeshuka kiwango cha ubora.


-NIMEJIANDIKISHA
-NIMEJIAPANGA
-NITATUMIA KICHINJIO CHANGU VIZURI
 
uko sahihi. kama jk anaondoka pamoja na kashfa zke basi sio mbaya kama lowasa naye akaongoza nchi yetu kama rais wetu.
 
Nafuu wewe umeamua kutoka CCM ili kuepuka dhambi ya kuwanyanyasa na kuwaacha wateseke Wananchi masikini wa Tanzania. Karibu UKAWA mpigie kura LOWASSA tuikomboe nchi kutoka kwa wanyonyaji na mafisadi wa CCM.
 
Ubarikiwe sana ! kasoro hizo awamu tu , lowasa kuwa rais wa kwanza baada ya ukombozi halisi ama wengine huita ukombozi wa pili .
 
Back
Top Bottom