Tulisikia mengi tangu kuanza kwa kampeni mpaka wakati huu tunasikia mengi juu ya nia nzuri ya awamu hii katika kuwaletea watanzania maendeleo.
Wananchi wote walijenga imani zao na matumaini yao juu ya awamu hii.
Hapa tulipo kama angekuwa mkulima angalau ungekuwa unaona shamba lililolimwa likisubiri kupandwa mazao pamoja na hapo watu wanajenga matumaini kuwa baada ya miezi kadhaa tutavuna.
Kama ni kandarasi wakati huu design zote zingekuwa zimekamilika, vifaa vimewasili saiti na mafundi wanakamilisha kazi za mwanzoni.
Lakini tunachojiuliza ni nia nzuri iko wapi kwa vitendo sio maneno ya kusema tuna nia nzuri?
Naweza kuchukua mifano michache
1. Suala la bomomoa kwa watu waliojenga maeneo yasiyofaa.
Ni jambo lililo wazi kuwa ujenzi holela katika miji yetu ni tatizo sana na ukizungumza ujenzi holela ni ujenzi usio na utaratibu. Chanzo cha ujenzi holela ni wenye dhamana kushindwa kutimiza wajibu wao wa kuweka utaratibu wa ujenzi katika miji.
Wananchi walitegemea serikali yenye nia nzuri ni kuanza kutimiza wajibu wake, kuweka plani za miji na kutumia plani hizo kupanga miji.
Lakini tulichokishuhudia ni kuvizia wahanga hawa waliotegemea kukombolewa kwa kuonyeshwa maeneo ya kujenga yaliyo sahihi, yanayowekewa utaratibu wa huduma za jamii hata kama hazijafika lakini watu wakae kwa utaribu wa kibinadamu.
Katika serikali ya awamu ya nne wakati amejiuzuru aliyekuwa waziri wa makazi na nyumba wa wakati huo niliandika kwenye mtandao huu kumuomba raisi uawaziri huo nikisema nilitaka kuanzisha programu ya kupanga miji yetu ndani ya miaka 15 miji yote itakuwa imepangwa. lengo langu halikuwa nipewe uwaziri kupitia anonymous identity bali nilitaka kuibua mjadala wa waziri anayeteuliwa apewe jukumu gani kama jukumu la msingi.
Leo hii tuna waziri wa ardhi anazungumza nchi nzima eti akigawa hati???? ni jambo la kusikitisha. miji yetu inazidi kukua bila mpangilio, kila mtu anajenga anavyotaka etu serikali inachokifanya ni kuhalalaisha makazi hoyo holela ili yapate hati yakopesheke na walipe kodi basi.
Nashindwa kupata picha kuwa serikali yenye nia nzuri haiwezi kuona kuwa usafiri ni ghali na wa shida kutokana na miji yetu kutopangwa, huduma za afya, masoko, shule yaani kila kitu ni shida kwa wakazi wengi kutokana na kutokapanga miji.
Wanaposema kupanga miji sijui tunatumia wahuni au wataalamu na kudai ni gharama kubwa ambazo hatuna eti mpaka tukakope benki ya dunia au sijui wapi, nashindwa kuelewa maana zaidi inaonekana kama matatizo yetu wengine wanayafanya dili.
Mantiki ya maendeleo ni kuwaunganisha wananchi pamoja kuwapa huduma kwa pamoja ili kuwapunguzia gharama za kupata huduma hizo na ndio maana unaambiwa mpango wa mji ndio hatua ya kwanza ya maendeleo.
Leo hii tuna miji iliyovurugika watu wanavuta maji kutoka zaidi ya kilomita moja, wengine wanaagiza maji kwa magari, wengine wanavuta umeme kwa kulipia nguzo tatu, mtu anapanda kipikipiki kila siku kufuata daladala na kurudi nyumbani hivi hawa tunawaongezea ughali wa maisha kiasi gani?
Utasemaje unashindwa kupata fedha za kupanga miji katika hali hiyo maana unapanga kwa wananchi kulipia kidogo na wakaepuka gharama kubwa za zinazotokana na makazi holela. A true leader lazima aone haya lakini wengine wataona dili za kukopa benki ya dunia. na unapotekeleza programu ya serikali yenye nia nzuri ni wananchi wanona matunda na sio kukopa fedha na bado wanaendelea kulipa gharama hizi au zinaongezeka nyingine juu.
2. Tazama mambo mengi watu wanalia ukata baada ya kuanza kutekeleza bajeti ya kwanza,
Tazama tunavyoshughulikia swala vilevi? je tunaibrand nchi yetu kwa vilevi au kweli tunapambana na vilevi?
Aliwahi kukurupuka mwandishi mmoja mtanzania akaandika samaki wa ziwa victoria wanavuliwa kwa sumu. matokeo yake ni samaki wote waliokuwa wakisafirishwa nje kule walikokuwa wakipelekwa wakazuiliwa.
Mwandishi huyu yeye aliona ni habari anaweza kuandika lakini sijui kama alijua madhara ya kile anachokiandika kwa nchi yake na je unaweza kuandika hivyo kama jambo limefikia hatua gani ili kuepuka kuleta madhara yasiyo ya lazima. Nakumbuka habari ile serikali ilitumia nguvu kubwa kujiosha kuwa uvuvi wa sangara wale hautumii sumu.
Lakini jambo hili linakuwa linatokana na nini?
Ni mifumo yetu ya elimu mibovu, unamchukua kijana unampeleka sehemu eti unamfundisha uzalendo kwa mazoezi ya mwili, kwa vitendo ambavyo ukiwauliza watanzania wote leo hii kuwa kuna uhusiano gani katika ya uzalendo na programu zile sijui kama wanaweza kulink.
Badala ya mtu kutambua kuwa uzalendo ni kuitumikia nchi yako au kutafuta mbinu za kuiletea nchi yako faida. hapa ni mtu kujua njia ambazo zinaweza kuleta faida na hasara katika jamii yake ili awe makini katika kuongea kwake asiikwaze nchi yake mbele ya mataifa mengine, katika kutenda kwake ajue anatakiwa kutumia fursa zilizopo katika jamii ili kuzalisha huduma au bidhaa kwa ajili ya nchi yake, mtu ajue anaweza uzalishaji wa bidhaa na huduma wa ndani na nje ya nchi ni wapi yeye anatakiwa kutafuta faida kwa nchi yake.
Leo hii tunakuwa na watanzania wanaoacha bidhaa za nchi yao na kukimbia kuagiza bidhaa za nje tena kwa kutumia fedha za umma na hao ndio wanaosikika kila siku wakihubiri uzalendo sijui kama hawa wanajua uzalendo ni nini? Watanzania hawa akitokea mtanzania anaona ana ujuzi wa kutengeneza bidhaa za nje watatumia njia zote kumzuia kwa kuziita bidhaa bandia hivi hawa wanajua uzalendo?
Leo hii kiongozi anaweza kukaa kwenye jukwaa na kuwadhalilisha viongozi wenzake, leo hii tunafanya mapambano ya ulevi kama mchezo wa kuigiza, kila mtu tunataja ni mhusika wa ulevi?
Sio vibaya kuwataja watu kama vyombo vyenye kuhusika na uchunguzi vimefanya uchunguzi na kubaini mtu fulani anahusika lakini haya sijui ni yaleyale ya minofu ya samaki au ni tofauti lakini tunaweka wapi uso wa nchi yetu kimataifa maana kwa sasa kimataifa itakuwa kila mtanzania anahusika na madawa ya kulevya. Nina uhakika kuanzia sasa mtanzania yeyote popote atakokwenda atapekuliwa mara mbili.
Ninaona tanzania tukiifanyia promosheni kuingia katika listi ya nchi za mexico na colombia kwa kufanywa na matamko ya viongozi?
Kama watu wanakamatwa na vilevi na tukafika huko sawa itakuwa tumejitakia lakini viongozi watatakiwa kufanya kazi kubwa kuondoa nchi yetu huko kwa kufanya juhudi za ndani kupambana na juhudi za nje kusafisha jina letu lakini sasa viongozi wanafanya kitu gani hiki?
Nikitazama mambo mengi nashindwa kutambua nia nzuri ya awamu hii iko wapi? Tutajiane matunda na sio michakato maana michakato inaweza kufeli hivyo tunapotazama nia nzuri tutazame matokeo.
Kwangu mimi tatizo naona ni watendaji kuona matatizo lakini hawana uwezo wa kuyatatua na matokeo yake ni kubuni suluhisho zinafanya matokeo tofauti na yale jamii inayotaka na kutumia nguvu ya nia nzuri ya awamu kuyasukuma na kusababisha mjadala mkubwa.
Awamu hii ijifunze kuwa jamii ikipiga kelele wasikimbilie kujijitetea kuwa wale waliokuwa wakienda kinyume ndio wanalalamika bali wajiulize suluhisho wanalolitoa kama ni sahihi. Jamii yenyewe itawapa majibu lakini upo uwezekano wa kutumia nguvu kubwa kushughulikia matatizo lakini baada ya miaka 5 kila mwananchi ni majeruhi na hakuna aliyechuma na kuisifia katika lolote.