The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,911
- 2,891
kumekua na shutuma lukuki dhidi ya mh paul makonda hasa kuhusiana na mpango wake wa kujaribu kupungunza makali ya maisha kwa waalim kwa kuwaomba wamiliki wa magari wakubali kuwasafirisha waalimu bure kama ilivyo kwa polisi na wanajeshi kwa bahati mbaya warusha shutuma wote inaonekana hawajui mipaka ya madaraka ya mkuu wa wilaya coz alicho kifanya makonda ni kutumia cheo chake kuona ni namna gani ana anapunguza changamoto za watu anaowaongoza cha kusikitisha ni kua kuna wakuu wa wilaya na mikoa ambao hata majina yao hatuwajui kwani hakuna wanalofanya kwa wananchi zaidi ya kusubiri matatizo yatokee na kuratibu ziara za kushtukiza za kina nape tuwashutumu hao kwani hawaonyeshi ubunifu wowote ikiwa kuna mpango mzuri zaidi mpelekeeni makonda ushauri ila kumbuka kua hana madaraka ya bajeti kuu anachofanya makonda anapaswa kupongezwa kwa kuthubutu hata kama hatuoni tija ukweli ni kua wengi wa wanaolalamika si waalimu na wengine ni wale wanaoishi karibu na vituo vya kazi hivyo kudhani hawatanufaika na huo mpango