Ni wapi wanafundisha kutengeneza pipi za kihindi?

Fateema

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2024
Posts
599
Reaction score
1,062
Enzi hizo baba angu alikuwa analangua kwa muhindi kariakoo.

Huyo muhindi alikuwa anazitengeneza kisha anawapa vijana wake kwenda kuuza kwenye mashule mbalimbali jijini Dar Es salaam lakini wakati huo huo akawa anawalanguza wafanya biashara mbalimbali, unaenda kununua kwake kisha unaenda kuuza shuleni.

Baba angu aliajiri vijana Saba kutoka Kigoma.

Alikuwa anaenda kulangua kwa muhindi kisha anawapa vijana wanaenda kuziuza mashuleni..

Baba angu alisimamishwa kazi mwaka 92 nipo darasa la kwanza akawa mjasiriamali wa duka, then tukawa tunatengeneza ice cream ( lambalamba) za kwenye mifuko vijana wakawa wanaenda kuziuza mashuleni..

Biashara ilitulisha hatukuwa na njaa ya chakula, but mwaka 94 friji likaungua na hatukuwa na means yoyote. Tulikuwa tunategemea friji tuuze barafu na mama alikua anauza dengu na visheti shuleni.

Dada yetu mkubwa ambae sasa hivi ni marehemu wakati huo alikuwa anasoma sekondari ndio alie introduce wazo la pipi za kihindi.

Shule ya msingi aliyo soma dada yangu kulikuwa na mtu ( mkaka) anauza pipi za kihindi za boss wake. Alikuwa anauza vibaya sana. Dada angu alikuwa ni mteja wa hizo pipi. Hilo la wazo la kutengeneza pipi za kihindi dada angu alilileta nyumbani mwaka 93 wakati tayari tumeanza biashara ya ice cream, ila baba alilikataa ( baba angu alikuwa mkoloni sana). Alilikataa kwa sababu alihisi ni mbinu za yule mkaka kuwa karibu na dada yetu.

So mwaka 94 maji yalipo zidi unga dada akaja tena na wazo hilo. Baba akalipitisha. Kazi ikawa tunazipata wapi au tunazitengeneza vipi. Dada kwa kutumia ushawishi wake alifanikiwa kumshawisui yule mkaka amuelekeze jinsi ya kutengeneza. Mkaka akamwambia hata yeye ameajiriwa anapewa hajui kutengeneza. Hata boss wake mwenyewe analangua lakini anafanya Siri kubwa sana hataki watu anapochukulia mzigo. Ila kupitia ushawishi wa dada yule mkaka alipeleleza hadi akapajua kwa huyo mhindi wanapochukua mzigo na baadae akaja kuwa mfanyakazi wetu akawa anaenda kutuuzia Sisi.

Baada ya kufanya hiyo biashara kwa Miaka miwili, baba aliona ni vyema sasa akajifunza ili azitengeneze yeye mwenyewe huku lengo likiwa ni kupata faida kubwa zaidi.

Kazi ikawa kumshawishi huyo mhindi kwa sababu alikuwa hataki kabisa kusikia kihusu ujinga huo( kufundisha watu)..

To cut story short, tulifanikiwa kujua namna ya kuzitengeneza pipi hizo kupitia mmoja kati ya wafanyakazi wake ambao walikuwa wanaenda kuziuza shuleni.

Again, Dada angu alihusika.. Dada alifanikiwa kumshawishi huyo muuzaji kumuunganisha na Moja Kati ya wafanyakazi wa huyo muhindi ambao walikuwa wanahusika na kuzitengeneza hizo pipi..

Jamaa aliitwa akaja kumfundisha baba ( Pepe yake). Baba hakutaka mama ajue wala mtu mwingine yoyote yule ajue jinsi ya kuzitengeneza.. Na akampiga marufuku Dada kuwa na ukaribu na huyo jamaa.

So alichokuwa anafanya baba kuanzia stage ya mwanzo hadi mwisho alikuwa anahusika Pepe yake. Sisi tulikiwa tunahusika wakati wa kuchomeka vijiti tu na kupakia kwenye mifuko, ambayo ni stage ya mwisho kabisa.

Biashara ilikuwa nzuri Sana. Baba alikuwa na wake wawili akaongeza na wake wengine wawili . Maisha yalikwenda vizuri sana baba alikuwa anaingiza hela zaidi ya waajiriwa wa serikalini.

Ila hadi anafariki, hatukuwahi kujua jinsi zinavyo tengenezwa hizo pipi..

Unajua mahali popote ambapo zinauzwa?

Unajua sehemu yoyote ambako wanafundisha namna ya kuzitengeneza?

Umewahi kuzila?
 
Hata akitokea mtu wa kuwatengenezea bado hamtajifunza kutengeneza wenyewe.Mnaonekana siyo watu wa kujifunza vitu.
 
Ndo tatizo letu watu weusi ndio maana hatuendelei. Wenzetu wanawarithisha ujuzi watoto na vizazi vyao pia formula zote zinaandikwa kwenye vitabu ili kutunza kumbukumbu. Ila kina sie sasa ni huzuni..
 
Unakufa na kihoro roho mbaya sana umejenga kijijini husemi mpaka siri zinavuja
 
Gazeti refu sana,hata wasahishaji wa mitihani wakiona hivyo huwa wanakata mstari mmoja mrefu kisha wanakwandikia 00!Jifunze kufupisha habari.
 
Enzi hizo baba angu alikuwa analangua kwa muhindi kariakoo.

Huyo muhindi alikuwa anazitengeneza kisha anawapa vijana wake kwenda kuuza kwenye mashule mbalimbali jijini Dar Es salaam lakini wakati huo huo akawa anawalanguza wafanya biashara mbalimbali, unaenda kununua kwake kisha unaenda kuuza shuleni.

Baba angu aliajiri vijana Saba kutoka Kigoma.

Alikuwa anaenda kulangua kwa muhindi kisha anawapa vijana wanaenda kuziuza mashuleni..

Baba angu alisimamishwa kazi mwaka 92 nipo darasa la kwanza akawa mjasiriamali wa duka, then tukawa tunatengeneza ice cream ( lambalamba) za kwenye mifuko vijana wakawa wanaenda kuziuza mashuleni..

Biashara ilitulisha hatukuwa na njaa ya chakula, but mwaka 94 friji likaungua na hatukuwa na means yoyote. Tulikuwa tunategemea friji tuuze barafu na mama alikua anauza dengu na visheti shuleni.

Dada yetu mkubwa ambae sasa hivi ni marehemu wakati huo alikuwa anasoma sekondari ndio alie introduce wazo la pipi za kihindi.

Shule ya msingi aliyo soma dada yangu kulikuwa na mtu ( mkaka) anauza pipi za kihindi za boss wake. Alikuwa anauza vibaya sana. Dada angu alikuwa ni mteja wa hizo pipi. Hilo la wazo la kutengeneza pipi za kihindi dada angu alilileta nyumbani mwaka 93 wakati tayari tumeanza biashara ya ice cream, ila baba alilikataa ( baba angu alikuwa mkoloni sana). Alilikataa kwa sababu alihisi ni mbinu za yule mkaka kuwa karibu na dada yetu.

So mwaka 94 maji yalipo zidi unga dada akaja tena na wazo hilo. Baba akalipitisha. Kazi ikawa tunazipata wapi au tunazitengeneza vipi. Dada kwa kutumia ushawishi wake alifanikiwa kumshawisui yule mkaka amuelekeze jinsi ya kutengeneza. Mkaka akamwambia hata yeye ameajiriwa anapewa hajui kutengeneza. Hata boss wake mwenyewe analangua lakini anafanya Siri kubwa sana hataki watu anapochukulia mzigo. Ila kupitia ushawishi wa dada yule mkaka alipeleleza hadi akapajua kwa huyo mhindi wanapochukua mzigo na baadae akaja kuwa mfanyakazi wetu akawa anaenda kutuuzia Sisi.

Baada ya kufanya hiyo biashara kwa Miaka miwili, baba aliona ni vyema sasa akajifunza ili azitengeneze yeye mwenyewe huku lengo likiwa ni kupata faida kubwa zaidi.

Kazi ikawa kumshawishi huyo mhindi kwa sababu alikuwa hataki kabisa kusikia kihusu ujinga huo( kufundisha watu)..

To cut story short, tulifanikiwa kujua namna ya kuzitengeneza pipi hizo kupitia mmoja kati ya wafanyakazi wake ambao walikuwa wanaenda kuziuza shuleni.

Again, Dada angu alihusika.. Dada alifanikiwa kumshawishi huyo muuzaji kumuunganisha na Moja Kati ya wafanyakazi wa huyo muhindi ambao walikuwa wanahusika na kuzitengeneza hizo pipi..

Jamaa aliitwa akaja kumfundisha baba ( Pepe yake). Baba hakutaka mama ajue wala mtu mwingine yoyote yule ajue jinsi ya kuzitengeneza.. Na akampiga marufuku Dada kuwa na ukaribu na huyo jamaa.

So alichokuwa anafanya baba kuanzia stage ya mwanzo hadi mwisho alikuwa anahusika Pepe yake. Sisi tulikiwa tunahusika wakati wa kuchomeka vijiti tu na kupakia kwenye mifuko, ambayo ni stage ya mwisho kabisa.

Biashara ilikuwa nzuri Sana. Baba alikuwa na wake wawili akaongeza na wake wengine wawili . Maisha yalikwenda vizuri sana baba alikuwa anaingiza hela zaidi ya waajiriwa wa serikalini.

Ila hadi anafariki, hatukuwahi kujua jinsi zinavyo tengenezwa hizo pipi..

Unajua mahali popote ambapo zinauzwa?

Unajua sehemu yoyote ambako wanafundisha namna ya kuzitengeneza?

Umewahi kuzila?
Interesting.
 
Nawe yamekufika kama yalivyomfika baba mkwe wetu mwaka 1992?
 
Back
Top Bottom