Tume ya Katiba
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 4,896
- 1,862
Kama kuna jambo lisilo na shaka kabisa ni kuwa JK na Membe ni mabigwa wa diplomasia, sio tu kwa kufanya kwao kazi wizara ya mambo ya nje kwa kipindi kirefu, lakini na uwezo wao mkubwa waliouonyesha kipindi wakiwa madarakani, kwa uwezo huo tumeshuhudia JK akiteuliwa kuwakilisha taasisi na mashirika mbali mbali ya kimataifa.
Ama baada ya kusema hayo, tokea huyu bwana Ngosha aingie madarakani kumekuwa na dalili zilizo dhahiri za kumweka mbali JK ikiwa pamoja na kutaka kuonyesha kuwa si lolote wala si chochote, tumeshuhudia kauli za dharau kwa JK kuonyesha kuwa hakuna alichofanya n.k........ Lakini kwa yaliyotokea ZNZ na matokeo yake kunyimwa msaada ni dhahiri kuwa hali si shwari.
Tokea tamko la kunyimwa msaada kumekuwa na panic ya hali ya juu toka kwa viongozi wa serikali akiwemo Magufuli mwenyewe, matamko mengi yanaakisi kukosekana wanadiplomasia wabobezi ndani ya serikali ya Magufuli. Kauli kama "Tutajitegemea", "Tulijiandaa" "Hatutishiki" "Tunajitosheleza" zimekuwa zikisikika sana miongoni mwa viongozi waandamizi wa Magufuli akiwemo Mh Magufuri mwenyewe. Kwa kweli kauli hizi sio za kidiplomasia, sio za busara na zimejaa kiburi. Kauli hizi zinaonyesha upungufu mkubwa wa "diplomasia" miongoni wa viongozi wa Magufuli.
Ushauri wangu kwako Magufuli, Taulo limekuanguka chutama......Kaombe ushauri kwa mwanadiplomasia aliyebobea JK na mweshimiwa Membe. Hawa watu ni werevu, watakusaidia ikiwa utaonyesha nidhamu na heshima kwao. Kwa sasa bado una hiyari ya kumfanya JK na Membe kuwa washauri wako wakuu.........
Kama ushauri huu hautaufanyia kazi, nikuhakikishie kuwa "Maalim Seif na Wafuasi wake" wamepata kick toka kwa "wadhungu" na muda si mrefu wataleta mtikisiko mkubwa katika taifa hili pale watakapoilazimisha haki kutendeka. Ikishafika hatua hiyo, utakuwa na machaguzi machache. Likishatokea hili, hutakuwa tena na hiyari juu ya ushauri wangu hapo juu, isipokuwa utalazimika kumfanya JK na Membe kuwa washauri wako wakuu...
Update 29-may-2016.
Seif atangaza kulianzisha.....
Niwatakie siku njema
Tume ya katiba (Mcheza Pool table maarufu)