Ni wakati wa kujitambua kama nchi juu Ya raslimali zetu

Escrowseal1

JF-Expert Member
Dec 17, 2014
4,540
4,505
Juzi nimekaa nikiangalia vichwa vya uingereza vinavyopambana juu Ya mstakabali wa hatima Ya nchi yao . Moja ni juu ya waliokuwa na Nafasi za utetezi kipindi cha Brixit campaign. Wengi wameishia kuachia Ngazi kwa Kuwa tu wamejitafakari kutofanikiwa kufikia malengo yaliyokuwa haja za mioyo yao. Mchakato wa kufanya negotiation ili kupata deal za ushirika kutoka jumuia Ya ulaya ni jambo ambalo mwingereza Hana mzaha nalo hata kidogo vivyo hivyo jumuia ya ulaya haina masiala Katika kuhakikisha inatoka na stake stahiki kama kutakuwa na negotiations hasa kuhusu uingereza ku access single market. Wakati mtangazaji wa BBC akireport yanayojiri kuhusu suala hili alisema sentence ambayo ki ukweli ilinivuruga kwa muda Kwamba - Negotions must be held by people who are on top of it. Maana yake kama nchi ni lazima ipeleke vichwa yenye uwezo vinavyoaminika kwani kama nchi ni lazima Ijitahidi ku maximize deal kutoka kwa umoja huo.

Nikija upande wetu na resources zetu tunazozidi kujaliwa kila kukicha hali inayotokea Kwenye hii community itupatie funzo hasa tunaponegotiate interest za Taifa . kama PM wa uingereza hajapata shinikizo hata kidogo la kuachia Ngazi ila mapenzi na uzalendo ndo inawapa msukumo. Si PM pekee ila wote mnajua wapo wengi wameondoka kutokana na uzalendo wao. Tumezoea resources nyingi kunegotiate na kubaki na kilio bila msaada. Mara uwazi wa mikataba hatuna, Mapato tunaambulia patupu nk hadi inafikia kipindi mwenye mamlka analia na very common person analia.

Ni lazima likifika suala la kunegotiate tutambue Kuwa ni vita na ki ukweli tujifunze wenzetu kila mmoja anavyosimama imara kuhakikisha deal linapatikana kwa manufaa ya Taifa . Mawaziri na wabunge hawana budi kufuatilia kinachoendelea ndani Ya jumuia ya ulaya Mfano . EU kulinda interest zake, uingereza vile vile na hata Scotland kuhakikisha haiburuzwi na ki ukweli hakuna anaemchekea mwenzake. Tume pata resources hasa ni Habari njema kwa Kuwa na Helium imepatikana ndani Ya ardhi yetu. Swali ni je tumejiandaaje kuhakikisha tuna maximize deal tukijifunza toka kwa jumuia ya watu wa ulaya ama bado hatujali hata tukitoka na deal kama la mh Mangungo. Kama nchi ni wakati wa kufanya kwa maslahi Ya Taifa . Resources kama Helium hatutegemei wanaohusika waweke mzaha hasa ku negotiate masilahi Ya nchi kwani ukiingia nchi za watu ukaona machines kama MRI zinavyookoa maisha Ya mamilioni ya watu ndo utajua Kuwa sasa na sisi ni wakati wa kutoka hata kama hatujakomaa kimatumizi ila ni dhahri kuwa bidhaa hiyo imeshazua taharuki kwa madaktari kwa Kuwa ni adimu sana duniani kwa sasa.

Mwisho tupate funzo hasa juu ya maslahi Ya nchi katika Jambo lolote na jumuia ya EU itupe fundisho kubwa naamini Raisi wetu kwa sasa ni wa kujivunia linapokuja suala la masilahi Ya nchi yetu . Wenye dhamana wawe wazalendo kwani dunia Ya leo kila mmoja anavutia kwake na wajue when the deal is completed in most cases ni irreversible na madhara yake yanakula vizazi. Naamini tutajifunza na siku moja tutafika.
 
Back
Top Bottom