Ni Wakati Sasa Majeshi Yetu Kujinadi Kisasa

Eagle One

Member
Dec 28, 2015
88
55
Hivi kwani Majeshi haya ya tanzania kuanzia la polisi, zimamoto, jeshi la wananchi yakifungua account kwenye mitandao ya kijamii kuna tatizo gani?

Dunia hii inaendelea na siku hizi ulimwengu wa utandawazi unazidi kua mkubwa kwanini tusifanye jeshi letu la kisasa na uboreshwaji huu hata hauna gharama ..

Kuna mambo ambayo ni lazima yabaki kua na usiri mkubwa ila kuna mengine ni ya kawaida tu ambayo unaweza kupost kwenye mitandao ya kijamii na raia wakajifunza baadhi vitu kijeshi .. Kwa maana jinsi wanajeshi wetu wanavyofanya kazi . jinsi wanavyo fundisha nidhamu .. Jinsi wanavyofanya kazi za mikono na mengine mengi tu ..

Nahisi hivi vyombo zinahitaji kuendelea sasa tuache habari za kuishi kizamani kwa maana hadi kusubiri maonesho wa sababa ndio ukaone uzalishaji unavyofanywa na JKT ..

Hii mada nadhani inahusu hata taasisi za umma zingine .. Tunahimiza utandawazi wakati serikali ipo nyuma sana kuendana na huo utandawazi ..

Hata hili shirika la air tanzania linalotaka kufufuliwa tusisubiri mpaka ukalipie matangazo kwenye machannel ya tv tu wakati pia wakati huo unaweza kutumia kujitangaza na kwenye mitandai ya kijamii pia, kwa maana tunatakiwa tukalipie kule kwenye tv na pia na wao wajifunze kukaa karibu na jamii .. ..
 
Naskia jeshi ni siri, mpaka iwe taifa stadium, ndio ruksa.


Ndio hapo sasa.. Kuna vitu havina ulazima kufanywa siri .. Sana sana tu itasaidia kuwapa mwanga raia kuona jeshi lao hua linawajibika kwa mambo gani maana kuna baadhi ya raia wanadhani wanajeshi hawana kazi za kufanya daily basis ..
 
Back
Top Bottom