Ni vizuri angeruhusu wapinzani wafanye siasa wangemsadia mkuu wetu

maganjwa

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
2,800
2,337
Mimi sioni mwisho mwema wa huyu mtu kwa kuwa naona hata hajui nchi ina matatizo gani katika wakati tofauti kupuuza shida na pia kukataa kama nchi serikali kutoa msaada kwa majanga sio sifa ni kujitakia matatizo makubwa mbele ya safari. Akumbuke umaskini wa nchi hii haukusababishwa na wtz bali rafiki zake ccm na viongoz wenzake waliptangulia kwa kushindwa kufanya mapinduzi ya fikra ya kuwatoa watu na kuchagua vema namna ya kukusanya nguvu ya watu ili wajiletee maendeleo wenyewe.
Angalia mawazo yake ya ajabu na yenye gharama kwake na ccm yake na taifa moja watumishi wa umms amewavunja morali ya kazi kwa kuwanyima stahiki zao bila sababu, ameshindwa kajiri wana wa nchi , anasingizia wafanyakazi hewa wakati hela hana, na sasa anatoa vitisho kwa watanzania eti hamna njaa ili hali utabir wa hali ya hewa umesema wazi mvua ndogo mwaka huu na kweli maeneo mengi haikunyesha na bado badala ya kuwa muungwana anasema njaa hamna na kuna watu wanatoa hela ili isemekane kuna njaa. Mimi nasema njia ya mwongo ni fupi na muda utasema kama anayosema ni kweli. Maana debe ya mahindi soko la kibaigwa ni 17000 arusha na manyara 14000.

Vitisho vyote ni kutaka asiulizwe serikali hii imeshindwa kufanya vitu vya msingi sana na kuhakikisha watu wananyamaza hata kama wanaumia je si kazi ya serikali kama kuna janga la kitaifa? na hata kama imetokea kwa bahati mbaya mfano tetemeko la kagera wanakagera walipenda tetemeko lije livunje nyumba zao ili waombe msaada? kwa nini wasimangwe kiasi kile juzi kati eti kuna mto ngono, mara katerero, mara ukimwi, nakadhalika kila kitu ni nyie tu sio uugwana hata kidogo tunajua ni katika kutafuta namna ya kuwanyamazisha wana kagera kwa machungu waliyonayo wasimuulize kwa nini serikali haikuweka mkono wake kama serikali ukitoa misaada.

Mimi naona kukimbia kivuli sio hakusaidii kitakufuata tu uugwana kukubali kwamba huwezi kukimbia kivuli na akubali rais ndo baba matatizo ya familia ni yake wala sio sahihi kumwandama mtoto mpaka unamnyima kula au kumnunulia dawa baada ya kuumia kwa kugongwa na baiskeli wakati anavuka barabara akitoka shule.

Hekima na busara inatakiwa hasa kama kiongozi wa nchi na hivi viwili (Hekima na Busara) ni zaidi ya sheria ndupo ubinadamu ulipolala ukifuata sheria peke yake wewe ni roboti wala sio mtu.

Hayo ni maono yangu ninaweza kuwa sahihi na pia ninaweza siko sahihi sana karibuni kwa mjadala
 
wakati nchi INA matatizo ya fedha wamemchotea lipumba na wenzie sh mill 360. alafu wanasema tuwe wazalendo tulips kodi,
 
Umenena vizuri, ujanja mwingi huondoa maarifa, muda utalonga!
 
Back
Top Bottom