Ni vita baridi kati ya Kikwete na Magufuli

Shondola

Member
Apr 2, 2014
95
58
#Mchakato ndani ya CCM Warejewa
# Gazeti la Jamhuri lahusishwa

# Kauli za Membe zazua gumzo

# Zanzibar kumbe ni Mtego

# Matamko ya Vijana wa CCM ni shida

# Kauli ya JPM Arusha yazua utata

# WanaCCM wasema Lowassa si tatizo bali ni CCM wenyewe

Ni takriban miezi miwili sasa tangu kuchaguliwa kwa ndugu Magufuli kama Rais wa Tanzania na utendaji wake umeendelea kuonekana na wako wanaouunga mkono na wengine wameendelea kuupinga na wengi wanaoupinga wameonekana kutoka nyumba ile ile aliyotoka Bwana JPM.

Hali imezidi kuwa mbaya baada ya kuanza kwa matamko mbali mbali toka kwa baadhi ya waliowahi kuwa Viongozi waandamizi ndani ya Chama na Serikali kutoa kauli mbali mbali dhidi ya Utendaji na Maamuzi ya JPM.

Maswali yamekuwa mengi kuhusu ni nini hasa kinachoendelea na yote hayo yametoka wapi. Chanzo cha kuaminika kimetanabaisha kuwa bado kuna kutokuaminika kwa JPM na yule aliyemwachia nafasi. Kwamba kimsingi Taifa hili linajua kuwa JPM hakuwahi kuwa chaguo la JK na wanaCCM na wale wataalam wa mambo ya kisiasa wanajua fika kuwa kudhulumiwa kwa Lowassa ndiko kuliko msaidia JPM kupenya katika kinyang'anyiro hicho na hili hata JPM mwenyewe analijua pasi na shaka.

Hivyo wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kinachoendelea katika Taifa sasa si kwamba JPM ana tatizo bali kile kiroho cha kutomtaka toka awali ndicho kinachomgharimu na ndicho kitakacho mgharimu manake asiyemtaka aendelee kumzunguka tatatibu.

Haya yakiwa yanaendelea chanzo chetu toka magogoni kimepata habari za ndani kuwa hata JPM mwenyewe aliyajua hayo toka awali na hata majipu anayoyatumbua ni yale yale ya yule asiyemtaka ili ujumbe umfikie vyema kuwa hata yeye JPM anajua fika kwamba hakuwa kumtaka ashike nyadhifa hizo.

Chanzo hichi kimeweka wazi kwamba ukitaka kujua JPM anafahamu vyema ni kuendelea kufuatilia yanayoandikwa na gazeti la JAMHURI. Chanzo hiki kimeweka wazi kuwa yote yanayoandikwa na Gazeti la JAMHURI dhidi ya Mstaafu na familia yanatoka moja moja kwenye nyumba nyeupe. Balile hakurupuki ana vyanzo vya msingi na ana mengi sana yaani bado ataandika sana na wanachoandika kina Balile yanatoka nyumba nyeupe moja kwa moja.

Chanzo hiki kimesema Balile ataandika mpaka Mstaafu atakapo amua kwenda Mahakamani na hata huko Mahakamani atashinda kwa kuwa ana ushahidi usiotiliwa shaka. Chanzo hiki vile vile kimesisitiza kuwa familia ya Mstaafu imelitaka Gazeti liwaombe radhi ila Balile hatafanya hivyo kwa kuwa aliyeko nyuma yake ana nguvu kuliko Mstaafu.

Katika kuendelea kuonesha kuwa ni vita baridi dhidi ya Mstaafu na aliyepo kauli za aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za nje imeendelea kuwa gumzo. Wataalam wa masuala ya Kisiasa wanasema kauli ya Mwanadiplomasia huyu ni kauli ya JK 100%. Si rahisi sana kutenganisha asemacho BM na familia ya Mstaafu. Hivyo ni wazi kuwa asemacho BM ni muendelezo ule ule wa vita baridi. Membe pia alisikika akipinga wazi wazi swala la ukubwa wa Serikali ya JPM kwamba bado hajapungumza chochote. Kauli ya Mwanadiplomasia huyu imekuwa gumzo sana Nchini na kushangaza walio wengi na Chama chake pia.

Si hivyo tu hali ya sintofahamu inayoendelea Zanzibar nayo imeonekana kuwa ni tatizo kubwa kwa Serikali ya JPM na hali hii imepelekea vile vile wachambuzi wa maswala ya kisiasa kuona kwamba kuna tatizo kubwa kutoka kwa Mstaafu kwani kinachoaminika kuwa toka mwanzo JPM alishasema yuko tayari kufanya kazi na wapinzani na hakuwa na tatizo lolote kwa Seif Shariff Hamad ila Mstaafu na wenzie wameendelea kuonekana kumzunguka JPM ili aendelee kuonekana tatizo ndani ya Nchi na Nje ya Nchi.

Kimsingi tayari Mataifa mengi yameshatoa misimamo yao dhidi ya yote yanayoendelea Zanzibar hasa baada ya kufutwa kwa uchaguzi wote Zanzibar. Jambo hili pia amelizungumzia Bwana Membe rafiki wa karibu sana wa Mstaafu akisisitiza kuwa Dunia inaishangaa Tanzania kwa hayo yaliyotokea Zanzibar.

Watu wengi wameendelea kumshauri JPM na Serikali yake wasione ukakasi wowote kutoa msimamo wao dhidi ya Zanzibar ni wakati wake sasa yeye JPM kuudhihirishia Ulimwengu kwamba naye ni mwana demokrasia wa ukweli na mpenda haki na wala hana shaka wala woga kufanya kazi na mpinzani yeyote. Na anapaswa kufanya hivyo kwa kuwa ni ukweli kwamba mshindi alishaonekana ila sasa kina wafitini wanaotaka kuufitinisha Ufalme wake ili aonekane si kitu.

Wasi wasi mwingine ulioendelea kuonesha sintofahamu ni baadhi ya matamko kinzani toka kwa Shirikisho la Vijana wa CCM na kilichoshangaza sana na pale mmoja anapotoa tamko hili na mwingine toka katika Shirikisho hilo hilo kutoka na kupinga na hivyo kushangaza umma dhidi ya uhalali wa hayo yote.

Haya yameshuhudiwa jana pale mtu aliyejulikana kama Salum Happy kiongozi toka Shirikisho la Vyuo Vikuu kutoka na kupinga kwa lugha kali kauli ya Bwana Membe na kumtaka amwache JPM afanye kazi yake. Lakini baada ya masaa kadhaa alijitokeza Bi. Zainab Abdallah ambaye inasemekana kuwa ndiye Mwenyekiti wa Shirikisho na kutoa tamko lake pia la kumpinga Salum Happy akisema kuwa tamko lile lilikuwa na Salum Happy na si la Shirikisho.

Hata hivyo baadhi ya watu ndani ya CCM wamesikika wakisema hivyo navyo ni Vita dhidi ya kambi za Urais kwa kuwa huyo Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bi. Zainab alikuwa na ameendelea kuwa mtiifu kwa Bwana Bernad Membe kwa kuwa yeye Membe na familia ya Mstaafu ndio walioshiniza Vikao vya CCM ili kuzaliwa kwa Shirikisho hilo kutokana na Familia ya Mstaafu na Membe kupoteza uhalali kwa Jumuiya ya Vijana (UVCCM) wakati wa uchaguzi hivyo wakaona bora kitafuta njia mbadala ndipo likaundwa hilo Shirikisho.

Salum Happy anasemekana kuwahi kuwa kambi ya Membe lakini alichukizwa na kuhamia kwa Pinda hivyo tamko lake naye pia limekaa kikambi zaidi na hataki kabisa kusikia jina Membe katika Siasa za CCM. Baadhi ya Vijana kutoka CCM wamesikika wakimwomba JPM afutilie mbali shirikisho hilo manake halina maana yoyote na si rahisi kwa Mwenyekiti wa sasa kufanya maamuzi dhidi ya Shirikisho hilo.

Jambo lingine lililoendelea kuwapa CCM wasi wasi ni kauli ya JPM aliyoitoa hivi karibuni akiwa Arusha pale aliposena inawezekana majipu mengi yapo CCM na Wananchi wengi kuonekana kufurahia kauli hiyo. Hivyo viongozi wengi wa CCM wengi wao wakiwa wamekwishawahi kutuhumia hata kwenye maswala ya ujangili wameendela kuonekana kuwa na wasi wasi na kupoteza imani kabisa na CCM. Mstaafu vile vile naye kapata shaka na hata swala la UDA kusemekana kufilisika imeendelea kuzua sintofahamu hasa ikizingatiwa ni majuzi tu Familia ya Mstaafu imehushishwa na Umiliki wa UDA. Haya nayo bado yanaendela kuonekana kuwa ni vita baridi vilivyoanza.

WanaCCM wengi walipoulizwa kuwa hawadhani Wapinzani wana mikono yao dhidi ya yote yanayoendelea kwao wenyewe wameonekana kukataa wakisema Wapinzani wala hawana Mkono na wamesisitiza kuwa wala hawataki kusikia kina Lowassa wanahusishwa na yote haya wameweka wazi kuwa Mhe. Lowassa kawa muungwana na kaondoka na wala hakutaka kufanya unafiki hivyo kama watasema ni Lowassa hata Wananchi watawashangaa tatizo liko ndani ya CCM wenyewe.

Wamesisitiza Lowassa yuko kimya na anafanya yake kama Mpinzania na ana heshima yake huko na kwenye Taaifa aachwe alivyo manake angeamua angeweza kubaki CCM na akatugharimu ila katoka na tunajua katoka bora yake yeye kuliko waliobaki halafu wanatoa matamko ya kipuuzi kama wapinzani. Wanasema haya mambo ya kila kitu kusingizia upinzani kuna wakati utafika watashindwa kujua adui yao kweli ni nani.

Wanakubali kuwa bado ndani ya CCM wapo watu wengi wenye imani chanya na Lowassa na huwaambii chochote dhidi ya Lowassa na wengine ni Viongozi waandamizi ndani ya Chama na wengine ni Wabunge ila badala ya kushughulika na hao watu waamgaika na Lowassa jambo ambalo halina mantiki. Mtazamo wao unabaki kuwa Chama hakiwezi kutetereka kutokana na nguvu za Wapinzani ila kutoka na madhaifu yao wenyewe.

Shondola Shekilango'
 
Mmh!?..Paragraph yako ya mwisho inatafakarisha juu ya andiko lako!??..inaashiria uko kazini..
 
eti mdhulumiwa luwasa...alidhulumiwa nini na nani?

nani asiyejua kuwa luwasa ndani ya ccm alishindwa kupenya na kukimbilia ukawa ambapo mdhulumiwa slaa alikimbia...na baadae luwasa kuhukumiwa na wananchi kwa kunyimwa kura takriban mil mbili?
 
Haidhuru uandishi umekaa kimipasho-mipasho na kuishangilia 'kwamba' iliyopo, ila ni kweli na dhahiri shahiri kuwa kuna 'damu mbaya' baina ya mstaafu na aliyemrithi. Imenidhihirikia zaidi katika matamshi ya Arusha. Ila sikushangaa, maana giza na mwanga haviwezi kuwa pamoja kwa wakati huo huo. Uchomozapo mwanga giza lazima likimbie na hivyo hivyo. Hata JPM angekuwa 'naive' kama hakutarajia hili kutokea.
Ah, nasema shabbaaaaash. JPM ongoza. Hii nchi si milki ya mtu yeyote ni nchi ya Watanzania wote. Wote tuna haki sawa. Hawa wanaotaka kuihodhi na kuiona ni yao, pambana nao na sisi tuko nyuma yako.
Ushauri wangu usiogope. Hili la Zanzibar ungesema mara moja kuwa haki ipewe kwa aliyeshinda, period. Kugwayagwaya katika hili kunakuondoshea sifa ya kuwa 'you are in control'. Kitu gani cha kuogopa na wewe uko katika haki na Watanzania wengi wanaliona hilo? Mbona huyo wao alipokuwa anatawala alikuwa anafanya maamuzi ya ovyo bila kujali mtu yeyote au hisia za Watanzania? Again, my advice: if you really want to 'lick up' Tanzania into shape, you have to be 'like a mad dog; too dangerous to care!' (a quote from a former Israeli Prime Minister, Ariel Sharon).
 
eti mdhulumiwa luwasa...alidhulumiwa nini na nani?

nani asiyejua kuwa luwasa ndani ya ccm alishindwa kupenya na kukimbilia ukawa ambapo mdhulumiwa slaa alikimbia...na baadae luwasa kuhukumiwa na wananchi kwa kunyimwa kura takriban mil mbili?
Hivi huoni kuwa huko ccm alidhulumiwa? Ni nami ambaye wanachama katika kura za maoni walimwamini na kumpa kura nyingi? Lakini hakupitishwa kwani majina wakikuwa nayo mfukoni
 
majipu yako CCM....VIVA Mr President. ..lowasa kakutuma kazi nzuri . nani hajui team lowasa ndiyo ilimpa kura Magufuli?
 
Back
Top Bottom