Ni vibaya kumwambia mke "JIONGEZE"?

Didododi

JF-Expert Member
Jul 21, 2023
321
426
Wanajukwaa mko pouwa?Huku ni pouwa ndyo napata lunch hapa NAPATA VITU VYA STUDIO PAMOJA NA MBOGA SABA (maisha si magumu kama mnavyozani)

Juzi bana nilikuwa kwa mshkaji wangu ambaye tunaivana sana .Shem katukaribisha chai pale wakati tunakunywa shem akamwita mzeiya nje.

Wakakaa muda kidogo huko mara ghafla nikasikia ugomvi kwa nje kumbe jamaa alikuwa anabananishwa aache kodi ya meza. Mhhh purukushani zikaendelea pale
======================
"Nimechoka bwana kunizongazonga kila saa hata vitu vidogo vidogo vya hapa ndani unashindwa kununua mbona wanawake wenzio wanaweza KA VIPI JIONGEZE" (Jamaa alipaza sauti)

Baada ya hapo mke alifura kweli "ahaa unataka nijiongeze ee haya bwana unachokitafuta utakipata"

Maneno yaliendelea kuwa makali akionekana kumtuhumu mumewe kumtaka ajiingize kwenye nyendo.

Sasa nikajiuliza hivi hauli kama hii tu inawezazua tafrani kiasi hiki.Wazee wa kudadavua hebu tujuzeni kuna shida hapo.

=========================
Kuhusu huo mgogoro nilitoka kuwaamua na kumwachia shem kama ten hivi la kutuliza machungu
 
Pumbavu kabisa, kujiongeza means fanya lolote, hata kujiuza, usikae na rafiki pumbavu kama huyo.
 
Kwa nini mgeni uingilie mzozo wa wenyeji wanandoa?
Suluhu ukaona uwe sehemu ya mgogoro kwa kutoa "li-teni"?
Badili tabia.Acha kuingilia mizozo ya wanandoa.
Umemdhalilisha jamaa yako ingawa mwanamke alifanya upumbavu kuanzisha mzozo huku "ugeni" ukisikia na kutaka kutwaa pointi za usuluhishi batili.
ANGALIZO:Usiwe mwepesi wa kutoa kauli za jumlajumla kwa mwenza wako/mke.Zinaweza kutafsiriwa vibaya na kuotesha mbegu mbaya ya dharau,kutokujiamini na usaliti.Mume usiruhusu mkeo kuanzisha mzozo wageni wakiwepo.Na uhakikishe mazungumzo yote yanaishia chumbani ambapo aliye nje asipate mwanya wa kuwasikiliza.
Vilevile,mdhibitiane kama wanandoa kutoanzisha mizozo wageni wakiwepo.Ni kazi ya mume hii kufanya udhibiti.Fanyeni maamuzi yenu pasipo kumuhusisha mtu wa tatu.Hata kununua nyanya muamuliwe na mgeni kwa kutoa li-teni?
 
Sasa mwanamke ajiongeze nini, jukumu la kuhudumia ni letu sisi, ikiwa ana kaajira sawa, ila hana ni wewe tu upambane.
Afe kipa,afe beki. Nyumbani waende chooni
 
Back
Top Bottom