Mwakaboko King
JF-Expert Member
- Apr 22, 2015
- 1,099
- 207
Kama tujuavyo Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa misingi ya Kidemokrasia, na mwisho wa Uchaguzi Mkuu mmoja ni mwanzo wa maadalizi ya Uchaguzi Mkuu mwingine. Matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 yalibainisha kuwepo kwa mwitikio mdogo wa wapiga Kura katika baadhi ya maeneo, kama mnakumbuka mwaka 2015 kulikua na hamasa kubwa sana ya wananchi kuwa na shauku ya kuwapigia kura viongozi wanaowataka katika ngazi ya Udiwani, Ubunge na Urais.
Kati ya wapiga Kura 23,161,440 walioandikishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ni wapiga Kura 15,596,110 ndio waliojitokeza kupiga Kura ikiwa ni sawa na asilimia 67.34. Wapiga Kura 7,565,330 sawa na asilimia 32.66 ya walioandikishwa hawakujitokeza kupiga Kura.
Hali hii imekuwa ikijitokeza katika chaguzi zilizopita tutazame mifano hapa
1. Mwaka 2000, waliojiandikisha ni 10,088,484 waliopiga Kura ni 8,517,998 (84.43%) na wasiopiga kura ni 1,570,886 (15.57%).
2. Mwaka 2005 waliojiandikisha ni 16,442,657 , waliopiga Kura ni 11,365,477(69.12%) Idadi ya wasiopiga Kura ni 5,077,180 (30.88%)
3. Mwaka 2010 waliojiandikisha ni 20,137.303 waliopiga Kura ni 8,626,303 (42.84%) na wasiopiga Kura ni 11,511,000 (57.16%).
4. Mwaka 2015 waliojiandikisha ni 23,161,440 waliopiga Kura ni 15,596,110 (67.34%) na wasiopiga Kura walikuwa 7,565,330 (32.66%)
MY TAKE: Kila Mtanzania anao wajibu wa kujitokeza kupiga Kura siku ya Uchaguzi, suala la watu kuishia kujiandikisha au kuhakiki majina yao halafu siku ya kupiga Kura hawajitokezi halikubaliki, wapo wananchi wanaopuuzia kwa makusudi kwenda kupiga Kura na hawa wamekua mstari wa mbele kuwalalamikia viongozi waliochaguliwa mambo yanapoenda ndivyo sivyo! jambo hili sio zuri, tunatakiwa sote kwa pamoja tuliondoe kwa kuhakikisha kila aliyejiandikisha anapata fursa ya kupiga kura 2020, Usiwaachie wengine wakuchagulie kiongozi.
KUPIGA KURA NI HAKI YAKO, MWAKA 2020 TUJITOKEZE KWA WINGI KUITUMIA VEMA HAKI HII.