Ni tendo gani jema?

Oscar Wissa

Senior Member
Joined
Sep 5, 2018
Posts
128
Reaction score
196
Sisi ambao tumeokoka, tunatakiwa kutenda mema, siyo ili matendo mema yatupeleke mbinguni, hapana!, tunatenda mema ili kuthibitisha uwepo wa neema na kumtukuza Baba yetu wa mbinguni.
Waefeso 2:8-9, Mathayo 5:16

Hakuna tendo lolote jema unaloweza kulitenda, litakaloweza kumshawishi Mungu akukubali na akuokoe.
Ni tendo jema moja tu ambalo linamfanya Mungu akuhesabu kuwa huna hatia, tendo la Yesu Kristo kufa pale msalabani.

Hakika kama Isaya asemavyo, hata yale matendo yetu mema tunayojisifia, mbele za Mungu ni kama uchafu tu.
Isaya 64:6

Ukiamini kuwa Yesu alikufa ili Mungu akukubali wewe na kukusamehe basi utaokoka leo!
Tendo la kupigwa kwake.
Isaya 53
 
Tendo jema ni kuupokea wokovu wa Yesu Kristo
 
We tafuta hela tu mkuu, ukizipata matendo yako yote yatakua mema.
 
Kutenda mema kwako si kuja hapa JF kubwabwaja, inabidi uende mitaani kutafuta watu wenye matatizo uwasaidie bila kujisifia. Unajuwa we Evangelist Oscar Maulid umetenda dhambi kubwa sana kuja hapa kutushawishi sie wasomi tunaojitambua wakati hatuna mpango nawe? Tafadhali tuombe radhi.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…