Ni suala la Muda tu

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,868
Reaction score
8,279
Marekani yawataka raia wake kuondoka nchini Urusi mara mo
Ubalozi wa Marekani mjini Moscow umetoa wito kwa raia wake kuondoka mara moja nchini Urusi kutokana na usajili wa wanajeshi wa zaida nchini humo

"Raia wa Marekani hawapaswi kusafiri hadi Urusi, na wale wanaoishi au wanaosafiri nchini Urusi wanapaswa kuondoka Urusi mara moja wakati fursa ndogo za usafiri wa kibiashara zikisalia," ubalozi huo ulisema katika taarifa.

Wanahofia kwamba mamlaka za Urusi huenda zisitambue uraia wa nchi mbili za Urusi na Marekani na kuwanyima watu wenye hati hizo kupata usaidizi wa kibalozi wa Marekani, kuwazuia kuondoka Urusi na kuwaita kwa ajili ya utumishi wa kijeshi.

"Tunawakumbusha raia wa Marekani kwamba haki ya kukusanyika kwa amani na uhuru wa kujieleza haijahakikishwa nchini Urusi. Epuka maandamano yoyote ya kisiasa au kijamii na usiwapige picha maafisa wa kutekeleza sheria kwenye matukio haya. Mamlaka za Urusi zimewakamata raia wa Marekani walioshiriki maandamano," ubalozi ulionya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…