Ni Sawa kwa marekani na nato kuivamia Libya kisha kupitia UN kemteua kikwete kumaliza mgogoro uliopo

Mpunilevel

JF-Expert Member
Sep 14, 2015
3,140
1,871
Salam, wanajukwaa.
Hii imekaaje hawa jamaa Ndio waliovuruga Libya kwa kuivamia kijeshi wakiwa na lengo moja tu la uporaji wa raslimali mafuta kwa kisingizio cha democracy
Nchi imeharibika vibaya, haitawaliki. Imejaa visasi baina yao na siraha zimetapanyika kila kona.
Wakati wanavamia hawa kutaka kusikiliza lolote mpaka azma yao itimie.

Nionavyo mimi katika mizozo, huu nimzozo mgumu sana. Na simkatishi tamaa Kikwete, kwa sababu kila jambo linawezekana kwa mipango madhubuti. Lakini ni kwa nini hawa super power wahalibu wenyewe halafu faida wakipata huitelekeza jamii hiyo?

Ni jukumu lao kuumaliza mzozo huu ikiwa pamoja na kushitakiwa kwa makosa waliyotenda. Sio kukiri walikosea halafu basi.

Mheshimiwa Kikwete hawa jamaa mzigo waliokutwisha ni ngoma nzito. Wameharibu sehemu nyingi tu kwa visngizio mbali mbali na wakipata hukimbia....

Nakutakia mafanikio kwenye hili.
Lakini?....
 
Back
Top Bottom