sifi leo
JF-Expert Member
- Mar 30, 2012
- 5,013
- 8,369
Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema, binafsi ninatambua kuwa sisi binadamu wote ni sawa na mazao tuliopandwa duniani na muda wowote ukiamua kutuvuna unatuvuna tyuuu majira yoyote.Nina tambua wanadamu kabla ya kifo chetu huwa tunaangaika sana kupingana na wewe Mola wetu usituvune.
Mungu wetu juma lililopita umewavuna mapacha walioungana hakika mimi niamini wewe umeamua kutenda lile wanadamu hatuwezi kulipinga wala hatuna nguvu hiyo! Sambamba, hayo yote nilitaka kujua Serikali yetu imepigania uhai wa watoto wetu vya kutosha?
Waliumwa mara ya kwanza wakalazwa huko kwao Iringa baadae wakaletwa Muhimbili wakapata nafuu, wakarudi huko kwao Iringa wanakaumwa tena na kurudishwa hapo hapo Iringa! Mpaka mauti yalipowakuta.
Sasa swali moja tu Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilipigania roho za watoto wetu vya kutosha?
Je kama walikuwa na tatizo la moyo kwanini hatukuwapeleka India ili wakatibiwe tatizo lipone kabisa?
Sawa wamekufa ila lazima tujiulize mchango wa Serikali kwa watoto hawa mpaka wanaaga Dunia katika hali za maumbile waliyokuwa nayo.
Pumzikeni kwa amani Consolata na Maria!