Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Bonyokwa amewaambia wananchi wa Kata hiyo kuwa ni ndoto kwa jamii yoyote ile duniani kote kufikiria maendeleo ya aina yoyote bila kwanza kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu ya barabara.
Mhe. Kuyeko ameyasema hayo Leo alipotembelea mradi wa ujenzi wa daraja linalounganisha Kata ya Bonyokwa na Kata ya Kinyerezi, daraja ambalo liko mtaa wa Kisiwani. Katika ziara hiyo ya kutembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa barabara kwa kata ya bonyokwa mhe. Kuyeko aliambatana na Afisa Mtendaji wa Kata hiyo ndugu Mtumbuka, wenyeviti na Afisa watendaji wa serikali za mtaa wa Bonyokwa na Kisiwani.
Aidha, katika kutembelea ujenzi wa daraja hilo ambalo ni LA chuma mhe. Kuyeko aliwakuta mafundi wakiendelea na kazi ya kuunganisha daraja, na Fundi mkuu alimuhakikishi kuwa kazi hiyo ya kuunganisha vyuma itakamilika ndani ya wiki hii na litaanza kutumika Mara moja.
Mbali na kutembelea daraja hilo mhe. Kuyeko na msafara wake walienda kuungana na mhandisi wa Manispaa ya ilala kukagua barabara za mitaa zinazokwanguliwa na kuwekwa sawa na Caterpillar la Manispaa.
Timu inayosimamia ukwanguaji wa barabara imeanza Leo kwenye mtaa wa Bonyokwa, itaenda mtaa wa Kisiwani na kesho watamalizia na mtaa wa Msingwa na ratiba ya caterpillar hilo kufanyakazi kwa Kata ya Bonyokwa itakuwa imekamilika.
Caterpillar hilo la Manispaa ya Ilala litazunguka kwenye Kata zote kuwangua na kurekebisha barabara zote za mitaa. Zoezi hili linafanyika kufuatia kamati ya fedha na utawala ya Baraza LA Madiwani kuidhinisha fedha ya mafuta ya caterpillar kwa ajili ya kukwangua barabara zote kwa Manispaa ya Ilala.
Baada ya ziara hiyo ya kutembelea miradi ya ujenzi wa barabara, mhe. Kuyeko alifanya kikao na wafanyakazi wote wa Kata na baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa za Kata hiyo. Kubwa alilolizungumza katika kikao hicho ni kwamba amewataka watambue kuwa wao ni watumishi wa umma hivyo jukumu lao kubwa nikuwahudumia wananchi wote kwa weledi.
Mhe. Kuyeko alisema Kata yetu ni mpya tunajukumu LA kuinje hivyo tufanyeni kazi kwa kushirikiana bila itikadi yoyote. Amewataka kujiepusha na rushwa na hatavumilia kuona wananchi wa Kata ya Bonyokwa na Ilala kwa ujumla wakionewa.
Imetolewa Leo 30/05/2016
Na Alex Massaba
Katibu wa Meya Manispaa ya Ilala.