singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
Baada kufanya ziara ya kushitukiza sikuJumamosi iliyowahusisha Mawaziri watatu wa Rais Magufuli, hapo alikuwepo Mwigulu Nchemba, Dk. Hamisi Kigwangalla na George Simbachawene walifanya ziara katika soko la Vingunguti na kufanya maamuzi ya kusimamisha baadhi ya watumishi kwa tuhuma za ubadhirifu.
Ziara nyingine imeendelea leo mkoa wa Pwani, Waziri Mwigulu Nchemba kafanya maamuzi ya kusimamisha watumishi wengine kwa tuhuma za ubadhirifu pamoja na kuamua kuzuia malipo ya Mshauri wa ujenzi wa machinjio ya kisasa iliyopo Ruvu mkoa wa Pwani.
Kingine ni kwamba Waziri huyo ameagiza Wajumbe wa bodi inayosimamiza ujenzi wa machinjio hiyo kuvunjwa siku ya Jumatano January 6 2016 kwa tuhuma za matumizi mabaya ya pesa.
Waziri Mwigulu Nchemba ameagiza pia kwamba anahitaji kupewa taarifa za mradi wa machinjio hayo pamoja na wabadhirifu wote kuwajibishwa.