Ni muda wa kusema kweli! Nini tatizo??

Travelogue_tz

JF-Expert Member
Sep 28, 2010
855
1,224
Ukweli usemwe sasa, Nini kikwazo katika Utoaji wa Ajira mpya na Upandishwaji wa Vyeo Na kulipa stahiki za watumishi? Bado tatizo ni Watumishi hewa ? Vijana wanateseka.

Ni takribani miezi 15 (Mwaka Mmoja na miezi mitatu) toka Rais JPM alipoanza rasmi utekelezaji wa majukumu yake kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku akiwa na historia ya kutoajiri watumishi wapya wala kupandisha vyeo wale waliopo kazini zaidi ya kufanya teuzi za kisiasa kama Mawaziri,Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Wakurugezi wa wilaya,miji na majiji, Mabalozi, Wakuu wa taasisi, Wenyeviti wa Bodi mbalimbali na Wabunge wa viti maalumu.
Mhe Rais mnamo tarehe 25 Octoba 2015 katika moja ya mkutano wake wa kusaka kura katika Jimbo la Kawe, Dar es Salaam akiwa kama Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM aliwahi kunukuliwa akisema mara atakapoingia madarakani serikali yake itakuwa ya kufanya kazi zaidi na kuwajibika kwa watanzania ambao wamekuwa wakilalamika mara nyingi juu ya utendaji wa baadhi ya watendaji wa serikali ambao hawawawajibika ipasavyo kwa taifa jambo ambalo linapelekea tija ya utendaji kushuka serikalini kwa sababu ya utendaji wa Michakato, “Serikali yangu haitakuwa ya Michakato au Changamoto Mimi kwangu ni Kazi Tu”
Tarehe 15 Machi, 2016 Mhe. Rais aliwaagiza Wakuu wa Mikoa na Waajiri wote kwa ujumla kuchukua hatua ya kuhakikisha katika Mikoa au Taasisi zao hakuna watumishi hewa ifikapo tarehe 30 Machi, 2016.
Kwa kusisitiza Zaidi, Mnamo tarehe 11 Aprili 2016, Rais alitengua uteuzi wa Mhe.Anne Kilango Malecela , aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa kashfa ya kutoa takwimu zisizo sahihi kuhusu idadi ya watumishi hewa ndani ya Mkoa wa Shinyanga.
Mnamo tarehe 23 Juni 2016 Mhe. Rais akizungumza wakati wa kuadhimisha miaka 50 ya Benki Kuu ya Tanzania, alisema kwamba serikali imeamua kusimamisha kwa muda usiozidi miezi miwili (2) zoezi la utoaji ajira mpya na upandishaji wa vyeo kwa watumishi wa umma ili kupisha uhakiki wa watumishi wa umma katika orodha ya malipo ya mshahara na kuondoa watumishi hewa. Na alisisitiza kuwa shughuli za kuwaajiri na kuwapandisha vyeo itaendelea kama kawaida baada ya kukamilika kwa zoezi hilo.
“Serikali ninayoiongoza haina nia ya kuwakatisha tamaa wafanyakazi, lengo lake ni kujipanga kwa makosa tuliyoyafanya, na ndio maana nimesema kwa kipindi cha mwezi mmoja hivi au hata mwezi mmoja na nusu, haitazidi miezi miwili, tusiajiri mtumishi yeyote serikalini’
’Katika kipindi cha mwezi mmoja hatutawapandisha vyeo wafanyakazi, ninaomba wafanyakazi waelewe hili, kwa sababu tukiendelea tutakuwa tunawapandisha vyeo hata wafanyakazi ambao hawapo, tunafanya ukaguzi wote tukishamaliza wafanyakazi wataendelea kupandishwa vyeo” alisema Rais Magufuli’:-Rais Magufuli
Mnamo tarehe 20 Agosti 2016, OMhe. Angellah J. Kairuki (MB.) Waziri wa nchi, Ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora, alitoa taarifa kwa vyombo vya habari kueleza umma juu ya utekelezaji wa agizo la Rais juu ya Watumishi hewa na kikubwa zaidi alitoa muda wa ukomo kwa ofisi ambazo bado hazijawasilisha taarifa ya watumishi hewa kufanya hivyo mpaka tarehe 26 Agosti 2016, Na Wizara yake itawasilisha taarifa hizo kwa Mhe Rais.
Mnano 18 Agosti 2016 Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa wilaya ya Ilala alinukuliwa akisema kuwa zoezi la uhakiki wa watumishi hewa limekamilika hivyo serikali itaanza kutoa ajira na kuwa watumishi waliopo ni halali.
Toka kutenguliwa , kwa Anne Kilango katika Ukuu wa Mkoa , na kuteuliwa tena kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yapata miezi 11 sasa imepita ( takribani mwaka Mmoja) lakini bado Ajira mpya hazijatangazwa, wala promotion hakuna na wala hakuna marupurupu ya watumishi .
JE HII NDIO HAPAKAZI TU ? AHADI YA KUMALIZA MICHAKATO I WAPI ? TATIZO NI WATUMISHI HEWA ? AU HII NI SABABU HEWA??
 
Anakera sana aisee,vjana 1 haisomek na 2 haikai kabsa! Tatzo nchi yetu imetawaliwa na siasa kila sehemu, uhakiki gani wa miez 8 huku mambo yote yakiwa yamesimama? Matamko na makanusho ndo yanayotawala, hao mawazr na wakuu idara nao ni hewa maana hawana sauti wala mawazo yakujenga!
 
Back
Top Bottom