Ni muda gani wanandoa wakae kabla ya kuamua kupata mtoto!?

G.Man

JF-Expert Member
Feb 9, 2014
1,022
2,065
Habarini wanajf, Naomba maoni yenu tafadhali, kukaa kwanza kwa muda kwenye ndoa ndo muamue kutafuta mtoto ama kuwahi kuzaa; ipi sahihi zaidi!?
Binafsi sijaoa na sitarajii kupata mtoto mapema baada ya ndoa, at least mwaka mmoja baada ya ndoa ndo mchakato uanze.
 
kila mtu na mawazo yake
ila mimi niliingia kwenye ndoa kwa jambo moja kuu
sikutaka kuzaa nje ya ndoa na nilikuwa nataka mtoto hasa hivyo mwandani wangu alijua hilo so wiki mbili tu baada ya ndoa akashika mimba
kuna jamaa yangu alikuwa malaya sana akatubia hivyo akutaka tena kuirudia zinaa na mwanamke aliyempata alikuwa bado yupo chuo plan kupata mtoto yeye ilikuwa mpaka apate kazi akishaajiliwa na jamaa ae pia alikuwa hataki mtoto kwa kipindi hicho wakakubaliana wakaja kuzaa baada miaka 3
mwingine kuna demu hapa kitaa aliolewa 7bu madem wengi hapa kitaa alocheza nao walikwisha olewa hvyo jamaa aliemuoa alimpa shart kuwa kushika mimba baada mwaka walikubaliana na wakaoana lkn ndani ya miezi 3 tu yule alikuwa na KIBENDI

ukifatilia hiyo mifano utagundua ni makubaliano ya wewe na mwenzako na nini unachofuata katika ndoa sidhani kama kuna muda maalum
 
Hakuna muda maalumu, ni nyie wenyewe mipango yenu,
Ingawa ni vyema mkaenjoy kidogo maisha ya ndoa just the two of you hata kwa mwaka mmoja ndio mkapanga kuanza familia,
Maana watoto wanachangamoto sana.
 
Hakuna muda maalum kama wote mko vzr, Kuna jamaa yangu mwaka wa6 ss anatafuta mtoto hapati
Muhim usije maliza watoto kwenye condom halafu wakati unawataka wakakosekana
 
Mkuu inatakiwa ndoa ianze kuzaa matunda piga kitu fasta, don't delay.
 
Habarini wanajf, Naomba maoni yenu tafadhali, kukaa kwanza kwa muda kwenye ndoa ndo muamue kutafuta mtoto ama kuwahi kuzaa; ipi sahihi zaidi!?
Binafsi sijaoa na sitarajii kupata mtoto mapema baada ya ndoa, at least mwaka mmoja baada ya ndoa ndo mchakato uanze.

Hakuna muda muafaka wa mtu kuamua kupata mtoto baada ya kufunga ndoa kwa sababu maamuzi hayo yapo mikononi mwa wana ndoa.

Ila kwa ushauri tu; si vyema kuchelewa kupata mtoto kutokana na sababu za kibaolojia na kiuchumi. Ni vyema ukapata mtoto mapema ungali bado kijana ili uweze kumlea vyema huyo mtoto na kumpa matunzo bora.
 
Inategemea unaoa ukiwa na umri gani? Sasa kama umevuta mke mwenye umri mkubwa weka mimba fasta
 
Nia yako kuoa ni nini? Kupata watoto au kupata papuchi ya bure karibu? Kama ni kupata mtoto, wahi mapemaa kabla ya jioni. Wanawake wengine huja kuleta mateso mengi kumpata mtoto hivyo ungejaribu kwanza mapema. Panga watoto unaotaka, zaa chap chap. Funga kizazi. Itamchukua mkeo miaka 4 tu kuteseka kulea. Baada ya hapo, mpo huru kabisa.
 
Kuna Braza angu, rafiki yake anakaribia mwaka wa pili now hana mtoto baada ya ndoa sasa huwa wanamdis sana nikifkiri me mwenyew sioni haraka ya mtoto mapema hvyo, nkamuuliza manzi wang yeye naye anasema hakuna kusubiri!
 
Hakuna muda maalumu, ni nyie wenyewe mipango yenu,
Ingawa ni vyema mkaenjoy kidogo maisha ya ndoa just the two of you hata kwa mwaka mmoja ndio mkapanga kuanza familia,
Maana watoto wanachangamoto sana.
Uko na point wewe, mkiwahi kuzaa hata tabia zenu halisi hamtaweza kuzielewa mapema alaf baadae muonane kama mmebadilika kumbe ndo mwenzako alivyo
 
Hakuna muda maalumu, ni nyie wenyewe mipango yenu,
Ingawa ni vyema mkaenjoy kidogo maisha ya ndoa just the two of you hata kwa mwaka mmoja ndio mkapanga kuanza familia,
Maana watoto wanachangamoto sana.
Mama uchumba wa miaka nane hamjajuana tu tabia ha ha ha ha ha
 
Kabla ya kuamua kupata watoto ni busara kwanza kuangalia kama kipato chako kinaweza kuwagharamikia coz ukishawapata asilimia kubwa ya kipato chako kitaenda kwenye malezi yao, kingine cha kuangalia ni lifestyle yako na mtu wako itabadilika/kuathirika vipi kwa kupata watoto na je mpo tayari kwa hilo?
 
Teh teh teh kama uchumba wa miaka 8, au wa kuishi pmj ndio mkaamua "kupasha kiporo" aiseee hapo hakuna budi ile mnamaliza Honey moon tu, ndoa iwe imejibu.
Ndoa nyingi za sasa ndo zipo hivo, watu washakaa wee wameishi wote wamezoeana styles zote wamemaliza ndo wanabariki ndoa..... Kuna haja gani ya kuchelewa kupata mtoto teh
 
Kabla ya kuamua kupata watoto ni busara kwanza kuangalia kama kipato chako kinaweza kuwagharamikia coz ukishawapata asilimia kubwa ya kipato chako kitaenda kwenye malezi yao, kingine cha kuangalia ni lifestyle yako na mtu wako itabadilika/kuathirika vipi kwa kupata watoto na je mpo tayari kwa hilo?
Sawa sawa kbs, maana kesi ni nyingi sana za wanandoa juu ya watoto.....

Tusiwatishe wengine.
 
Back
Top Bottom