Ni mtazamo tu wadau

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
69,876
183,917
Habari wadau,
Ufisadi umekuwa ni msamiati uliotamalaki zadi kwa takribani miaka kama kumi sasa hapa nchini, nipongeze juhudi za serikali kuliona kuwa ni jambo lisilopendeza kuendelea kuwepo na sasa wameanzisha mahakama ya mafisadi na wahujumu uchumi!
Nimekuwa nikitafakari sana juu ya hili swala na binafsi naona chimbuko lake ni katika system ya ajira za serikali.Nina mitazamo tofauti sana ambayo inaweza kusaidia sio tu kuoverride hili swala ila pia kuongeza ufanisi though i stand to be corrected.

1.Kwanza ningependekeza system ya kuajiri watu serikalini na sheria zibadilike na kazi ziwe za mikataba ya muda usiozidi miaka 3. Baada ya mkataba huu kuisha watu watalipwa stahili zao na kuwa offered kwenda kuwa walimu wa vyuo vikuu wakienda kufundisha utaalamu wa yale waliofanyia kazi.Wale watakaokuwepo vyuoni watapisha kwenye safu na waende wakajiajiri sekta binafsi maana watakuwa na uzoefu wa kutosha .Hii itaondoa dhana ya watu kuzeekea serikalini na kuona kuwa nafasi walizonazo serikalini ni sehemu ya kupumzikia au kuchuma na si sehemu ya kufanya kazi kizalendo. Mafisadi wengi ni zao la kukaa kwenye system ya serikali muda mrefu sana na huambukiza hii tabia kwa vijana wapya wanaokuja wakiwa wazalendo hatimae nao wanafundishwa udokozi so its becomes a cycle.

2.Mtumishi apewe mkataba mzuri wa kazi, uambatanishwe na master plan ya kazi na targets anazotakiwa kuzifikia kwa wakati wote atakaokuwa kibaruani.
Kila senior officer wa serikalini ni lazima alipwe kwa haki ila pia atatakiwa aweze ku perform ili kufikia malengo na asiwe goigoi katika nafasi aliyopewa obvious tutahitaji na ka mfumo ka kuwa assess hawa watumishi.Ikiwa kama mtu huyu hataweza kuendana na kasi ya kufanya kazi alizopangiwa ili afikie malengo basi kutakuwa hamna namna zaidi ya kumpiga chini maana wasomi tunao wengi.Zile element za kulea uzembe na nepotism zitapungua ambazo nyingi zimepelekea ufisadi wa kutisha serikalini.

3.Kuwekwe sheria kali ya watumishi watakaobainika kufisadi au kuhujumu uchumi,
Nadhani mahakama watakuwa na mamlaka na hili zaidi.Mtumishi yeyote wa serikali atakaebainika kuhujumu uchumi kwa namna yeyote hata kama kadhulumu jero tu ningependekeza apigwe mvua za kutosha bila dhamana.Ikiwezekana mtu asionekane uraiani hata miaka 40, na hio ndio itakuwa fundisho na kwa vile atakuwa ni kijana akirudi uraiani akakuta wajukuu sio mbaya!

4.System ya kupata waajiriwa iwe ni kusomesha vijana wetu katika nyanja tofauti hapa serikalini, wachukuliwe cream students top 5 katika kila shule tofauti za vipaji maalum waliokuwa assessed for years kama wafanyavyo TISS. Hao ndio watakwenda kushika senior positions serikalini na kwenye mashirika! Walipiwe gharama zote wasomeshwe vyuo vizuri huko ughaibuni wajifunze jinsi wenzetu wanavyofanya mambo yao na kupata maendeleo ili wakitoka huko waje kufanya mambo practically, watakuwepo automobile engineers, wawepo pilots, managers na kadhalika ambao wataweza kuapply knowledge zao vizuri katika kumudu mashirika na viwanda tutavyoanzisha bila kusababisha hasara ama kuviua kabisa. Ikumbukwe kuwa kama kazi itakuwa ya mikataba itakuwa ni rahisi ku phase out obsolette ideas maana kila baada ya muda mchache watumishi wanabadilika completely inaingia intake mpya ya vijana.
 
hhiyo kazi ilimfaa huyu jamaa maana yuko na vision ya uongozi na yuko karibu na walala hoi.
images-18.jpeg


swissme
 
Back
Top Bottom