Ni mchakato gani unaofanyika katika mwili hadi mtu anazeeka?je kuna uwezekano wa kuzuia uzee ?

JITU LA MIRABA MINNE

JF-Expert Member
Mar 28, 2015
726
475
Wazee turejee swali hapo juu,utadhibiti vipi uzee ?je kwa mazoezi,vyakula,style ya maisha au nini hasa?nahtaji kuwa na body yenye ukakamavu na nguvu hata miaka 90 nikijaaliwa kufika nafikiri kila mtu ana malengo hayo
tupeane nyepenyepe,ronger,dondoo,ili tuendelee kula bata karibuni wajuzi,madokta na wataalam wa viumbe hai uwanja wenu
 
Uwezekano huo upo, sema sasa unatakiwa utambue lazima utakufa tu,
na kama unavyojua huwa tunaishi maramoja sasa itakuwa haimake sense eti ujitese weeee then mwishowasiku unakufa bila hata kuishi( unapokuwa duniani Usisahau kuishi).
Ninaposema kuishi namaanisha hapa duniani kuna watu wanaishi na wengine wapowapo tu,
Mtu utakuta yeye tangu kijana anatafuta hela weee mpaka anazeeka anakufa kwa stress za hela,
sasa mtu huyo hatumuhesabii kama ameishi.
Mfano mzuri wanyama wa porini wale wanaishi,...(ukiwa na swali uliza)
Sasa tukirudi kwenye mada yako, mbinu pekee ya kuishi muda mrefu inaanzia tangu ukiwa tumboni, kama mzazi wako akibugi tu basi unakuwa hauna maisha marefu, na baada ya kuzaliwa unatakiwa ufuate kanuni isemayo AFYA YAKO YA KESHO ITATEGEMEA NA UNAVYOISHI LEO.

...ngoja niishie hapa,
 
kuna watu husema chumvi, ngono ya mara kwa mara,na vyakula vyenye mafuta huleta uzee hapo nimetoa summary tu ya niliyoyapata na nyie muongeze nyama
 
Uzee ni hali ya Kibaolojia hii ni lazima kwa vitu vyote vyenye Uhai.

Mazingira na Mtindo wa maisha ndivyo vitakavyokufanya uishi miaka mingi.
 
Hujabainisha mbinu ya kuzuia uzee apo wapo wanaosema chumvi husababisha uzee sasa toa mawazo yako
Kuzuia uzee haiwezekani. Ni sawa na kutaka ukipanda mahindi yakishaota yabaki kijani bila kukomaa na kukauka hapo hatuwezi kuvuna. Nawe binadamu lazima uzaliwe ukomae uzeeke halafu Mungu avune. Ndo maana ya uhai.
 
Rudi utoton, ukishndwa kutembea utabebwa mgongoni.
Hyo ndo dawa pekee ya kuzuia uzee.
Ni kama wezi wanaojtambua huiba mpaka cku ya 39 na kuanza 1 tena hawafikishi 40
 
Uzee ni lazima hata usipokula chumvi, usile mafuta lazima utazeeka tu, tukikataa uzee tukatae na watoto wachanga kukua.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom