Ukweli ni kwamba VIP ililipwa kwa msingi wa Mkataba wa Uuzaji wa Hisa uliotangazwa na kuridhiwa kwa amri ya Mahakama ya Septemba 5, 2013; na kufuatiwa na amri ya mahakama ya Januari 17, 2014 iliyotolewa katika shauri la wazi; na baada ya kuwa imefanya malipo ya shilingi za Tanzania bilioni 38 { sawa na dola za Marekani Milioni 23.6} katika Mamlaka ya Mapato Tanzania {TRA} kwa ajili ya kugharimia malipo tote ya kodi ya VIP. Kwa ujumla VIP ilipokea fedha kwa mauzo ya hisa zake iliyokuwa imeruhusiwa kuziuza; mauziano hayo na malipo yalifanyika kwa uwazi mkubwa na kwa ruhusa ya mahakama na VIP si tu kwamba imeahidi kulipa kwa ukamilifu kodi zozote zile bali tayari ilikwisha kukabidhi TRA shilingi Bilioni 38 kama kodi mbalimbali kutokana na mauzo hayo.