NI lini watumishi raia wataondoka jeshi la polisi?

wwww

JF-Expert Member
Mar 20, 2012
350
252
Ni muda mrefu umepita tangu mtukufu sana Rais kumwagiza IGP kuwaondoa watumishi raia Jeshi la Polisi, lakini taarifa zilizopo ni kwamba hakuna mtumishi hata mmoja ambaye ameondolewa.

Sasa hii inamaanisha kuwa kauli za Mtukufu sana Rais zinapuuzwa na watu wake na kuamua kumpotezea au ni nn sasa?

Ukiangalia clip ya siku mtukufu sana Rais alipotoa tamko la kuwaondoa watumishi raia Jeshi la Polisi IGP pamoja na makamishina wengine walishangilia sana kwa jambo hilo lakini mbona hawatekelezi agizo la Mtukufu Rais?
 
Kabla ya kuwaondoa inabidi kufahamu taaluma zao na sababu za kuajiliwa kwao!

Lakini pia kama kigezo ni wao wawe askari wale wenye umri unao weza kwenda mafunzoni wanaweza pewa special program wakawa askari.

Pia sheria ya kazi na sheria ya jeshi la polisi inaongea nini kuhusu sababu za kumuondoa mtu kazini? Yote haya lazima yaangaliwe ili kuepusha msururu wa kesi mahakama ya kazi na fidia zisizo za lazima.
 
Back
Top Bottom