Baada ya kufanya uchunguzi kwa Muda Mrefu kuhusiana na Simu ipi ya Android ni bora na yenye Ufanisi, nkagundua kuwa LG G2 ndio simu inayoongoza kwa ubora na Ufanisi Duniani japo watu wengi wameshanyweshwa maji ya Bendera ya Samsung na kuziona kuwa ndio simu/smartphone nzuri.
Mitandao mingi inayochunguza Consumer products Kama CNET/Gsmarena na Mingineyo imeweza kutambua uwezo wa Simu za LG na kugundua kuwa, wale wote walionunua simu za LG especiallyy LG G2, walikuwa na kila sababu ya kutabasamu baada ya kupata thamani ya Pesa zao mara baada ya kununua simu(LG G3).
Watu walio wengi hivi sasa wanaisubiria kwa hamu kubwa sana toleo lao la 3. Yaani LG G3.
Binafsi sijawahi kutumia Android. Nmekuwa nkitumia Blackberry for the Past 6years na nikawa satisfied na utendaji kazi wake. Ila binadam lazima tuwe/tuenende na Mabadiliko. Nikaona sio vibaya nishift toka BB na nitafute Android Device ili nami niweze kuwa familia kwenye ulimwengu wa Android.
Kabla ya kununua mojawapo ya Android device,nikaona nifanye uchunguzi juu ya simu gani ya Android ambayo nikinunua sitajutia kwa nini nimehama BB.
Baada ya Uchunguzi nikagundua kuwa,for the tyme being, Simu Bora Duniani kwa Sasa yenye Android technology ni (LG G2) Nikashawishika kwenda kuinunua. Kuna jamaangu Mhindi town huwa napenda kununua vitu vya Elektonics dukani kwake. Nlipofika nkamwambia nnataka kununua "LG G2" akanambia "kwa nini usiwe mvumilivu kwani toleo jipya LG G3 liko mbioni kutoka!?" Nikafuata ushauri wake.
Kwa yoyote mwenye taarifa za lini ujio wa hii Simu, tupeane taarifa kwenye huu uzi.