Ni lazima vijana wakimbilie kuajiriwa

Maserati

JF-Expert Member
Jun 15, 2014
11,604
20,079
Habari zenu wana jamvi,
Kila siku ninakaa ninafikiri na kutafakari baadhi ya vitu ninavyoviona kipindi hiki chote cha maisha yangu. Na hiki ni kimoja wapo.
Inafika kipindi lazima tuseme ni lazima vijana wasubiri na kukimbilia kuajiriwa. Hali inakuwa ngumu kiasi kwamba vijana wanashindwa kujiajiri, sababu kuu ikiwa ni mtaji.
Utakuta kijana ana wazo zuri sana la biashara, lakini mawazo yale yanashindwa kuwa implimented kwa sababu ya mtaji.
Mtaji ni msiba nzito sana kwa vijana wa sasa katika nyanja hii ya kujiajiri. Unaweza kufikilia kuchukua mkopo, lakini hakuna biashara inayofanikiwa kwa kutumia pesa ya mkopo kama kianzio cha biashara. Nyingi zinakuwa na changamoto sana mpaka kufikia kuporomoka na kufa, huku muhusika akibaki na deni la kulipa., headache.

Kuwa na kianzio chako, changanya na pesa ya mkopo fanya biashara. Lakini, mikopo hii ina masharti yasio rafiki kwa vijana, especially kwenye upande wa udhamini wa mkopo wako. Ataweka dhamana gani apate mkopo wa kukidhi hitaji lake? Hapa wengi wanakosa sifa za kupata mikopo, na pengine kupata kiasi kidogo sana ambacho hakikidhi mahitaji ya mtu husika.

Na sio kama hatufahamu, lakini utashangaa sana mtu anamwambia kijana jiajiri usisubilie ajira wakati huo katoka kukuomba mia 500 ya nauli. Unamtangazia kujiajiri. Real?? Au wakati huo unaona life stlye yake ilivyo ya kusua sua hapo mtaani.

Sikatai kwamba inawezekana and i believe on kujiajiri, lakini mitaji ya kuanzia biashara na ujasiliamali ndio shida kubwa sana kwa sasa.

Usimlaumu mtu unapomuona yupo idle, anasubiri ajira za serekali zitangazwe.
Hii dhana ya kujiajiri ni nzuri, lakini inakosa mashiko kwa vijana wengi ambao inawahusu na kuwagusa vijana wachache.

Wakati huo huo wapo ambao wana uwezo kabisa wa kupata mtaji na kujiajiri, lakini tatizo huja kwa sababu ya kukosa mtaji wa mawazo na uwezo wa kufikiri. Wasaidiwe, na sio kuwasema vibaya au kuwacheka. Toa msaada kwa yule ambae unaona kabisa ukimshauri atautumia ipasavyo ushauri wako na utakuwa na manufaa kwake, atauchukulia positively na kuufanyia kazi. Achana na watu wenye negativity ideologies.

So, kutokana na bandiko hilo hapo juu, nashauri, Usimlaumu wala kumkejeli kijana anae subiria ajira ikiwa unafahamu hana uwezo wa kujiajiri. Kwa kumsaidia, mpe taarifa ikiwa nafasi za kazi zimetoka.

neno langu si sheria, lakini akili za kupewa changanya na za kwako.

Ramadan kareem.
Kazi na utafutaji mwema.
 
Kinachotukwamisha vijana wengi wa Tanzania ni mifumo yetu ya taasisi za kifedha ambazo zina sheria na taratibu ambazo si rafiki kwa mchukuaji mkopo, kuna mchangiaji hapo juu nmeona anasema wazo lako ni mtaji huo ni ukweli hatuukatai lakini kama ni wazo ambalo linahitaji fedha iliyokuzidi uwezo wa kuwa nayo kwa wakati huo mawazo mengi huwa ni mfu.
Kikubwa nadhani kuna haja ya kuitizama tena mifumo ya taasis zetu za kifedha kwenye swala zima la kutoa mikopo kama kasumba zilizopo zitapatiwa ufumbuzi haswahaswa kwenye swala la dhamana ya mkopo nadhani watu/vijana watakuwa wamepata ukombozi ila kwa sasa si rahisi ila inawezekana kujikomboa.
 
Kinachotukwamisha vijana wengi wa Tanzania ni mifumo yetu ya taasisi za kifedha ambazo zina sheria na taratibu ambazo si rafiki kwa mchukuaji mkopo, kuna mchangiaji hapo juu nmeona anasema wazo lako ni mtaji huo ni ukweli hatuukatai lakini kama ni wazo ambalo linahitaji fedha iliyokuzidi uwezo wa kuwa nayo kwa wakati huo mawazo mengi huwa ni mfu.
Kikubwa nadhani kuna haja ya kuitizama tena mifumo ya taasis zetu za kifedha kwenye swala zima la kutoa mikopo kama kasumba zilizopo zitapatiwa ufumbuzi haswahaswa kwenye swala la dhamana ya mkopo nadhani watu/vijana watakuwa wamepata ukombozi ila kwa sasa si rahisi ila inawezekana kujikomboa.
Asante ssna mkuu.
This is naked truth yaani iaseee
 
hii imekaa vizuri naunga mkonyo (mkono) hoja ila relato angekuja tupate mawazo yake ingekaa vizuri zaidi hebu mwite
 
Tatizo co vijana ni mfumo wa elimu, elimu ya tanzania inamwandaa mwanafunzi kuja kuwa mwajiliwa hakika nikipata chance ya kuwa rais wa nchi shule zote nageuza veta ni kusoma fani tu
 
Kubali kataa. We njoo na idea yako ya kijasiliamali. Halafu uwe huna hata mia, kama hutokaa na mind set yako till to the grave
3efeb207d772eec68350e96dca785e2b.jpg
 
Back
Top Bottom