Ni Lazima timu za Vijana kuwa na kocha wa Kigeni?

NG'OTIMBEBEDZU

JF-Expert Member
Aug 11, 2010
1,180
592
Kwa wale wapenzi wa Soka Bongo,naomba tulijadili hili.
Binafsi sioni kama kuna ulazima wa kuwa na kocha wa kigeni ktk youth ranks e.g U17 au U 20,kwa sababu naamini tunao makocha wa hapa nyumbani wenye uwezo wa kuzinoa hizi timu,mradi tu wapewe mikataba ya kueleweka, wapate vifaa na support nzuri ya wadau.
Kwa mfano,tunaweza tunaweza kumpa Mohammed Rishard "Adolf"afundishe U17 kwa kushirikiana na Mbwana Makata, vilevile tunaweza kumpa Sylvester Marsh afundishe U20 akishirikiana na Rogatius Kaijage.
Nimefuatilia na kuona kuwa hawa ma-TX wetu licha ya kupewa hela ndefu,bado mafanikio yao hayaridhishi,kwenye youth ranks.
 
Mkuu nakubaliana na wewe kabisa. Hayo mapesa tunayowapa hawa makocha wa nje tungeweza kuyatumia kuwapa ajira ya full time makocha wazawa na ambao wanauwezo mkubwa sana. Kwa mfano pale a-town yupo mzee ally mtumwa, ambaye amekuwa mstari wa mbele sana kuendeleza soka la vijana pale mjini, lakini anaangaliwa kama nyanya mbovu.
 
Lakini kaka ajila ya ukocha inafuata experiance ambayo mutu anayo katika medani ya kimataifa,kisha achieve nini kwenye medani ya michenzo.Ukiangalia hapa Tanzania hatuna makocha wenye uzoefu wa kimataifa waliofanya vitu vya kueleweka.
 
Lakini kaka ajila ya ukocha inafuata experiance ambayo mutu anayo katika medani ya kimataifa,kisha achieve nini kwenye medani ya michenzo.Ukiangalia hapa Tanzania hatuna makocha wenye uzoefu wa kimataifa waliofanya vitu vya kueleweka.

Uzoefu upi wa kimataifa? au na wa kwetu nao wakafundishe Ulaya? Hawa makocha wa hapa nyumbani tayari wana exposure na experience nzuri tu kimataifa.
Tunachopaswa kukifanya ni kuwaamini na kuwapa timu.Kibadeni aliweza na Serengeti boys,kabla y disaster ya Nurdin,Marsh kaenda na timu ya Copa Cocacola Brazil akarudi na ushindi,licha ya hivyo elimu yao ya ukocha na mafanikio yao ktk kazi zao tunyaona,tuwape mikataba ili wajiamini kuliko hivi tunavyowatumia kama dei waka.
 
Hayo ndio matatizo ya Waafrika. Tunathamini kila kitu cha mzungu kuliko vitu vyetu wenyewe, hata vyakula, mf. Mayai ya Kizungu mpaka leo yanaonekana bora kuliko ya kienyeji wakati kiafya sio kweli. Keshi kutwa utasikia Tanzania wamepata kocha kutoka Canada, pamoja na kwamba wao pia ni midabwada. :sleepy:
 
tatizo sio mgeni au mzawa,inatakiwa taaluma umesoma kabisa,sio ukocha wa blah blah au sijui kacheza mpira,hapana,ukocha unaingia darasani unasomea mchezo na kuubadilisha,kusuka timu,kuitengeneza,kuwajenga pamoja kisaikolojia nk,sio kazi rahisi tunavyodhani,sasa hapo ndio tuangalie makocha wenye sifa japo sio sawa kama wenger,ferguson,mourinho,ancellotti,hiddink,van gaal,ottmar hitzfeld,vicente del basque,bert van marwijk,marcelo lippi,trappattoni nk,wanazo sifa hizo,kupitia rekodi zao hasa hasa kimataifa.
 
Back
Top Bottom