kitu ambacho mnapawa kukielewa wakuu,Simba hii ya sasa ,Jina lake tu kibiashara linathamani ya hiyo pesa,twende mbele turudi nyuma wanachama wa simba na mashabiki wa simba wengi wenu mnapelekeshwa na kivuli cha utajiri wa Mo Dewji,sawa sikatai kuingia katika mfumo huo,lakini iwe kwa thamani halisi ya klabu,Simba ni mgodi unaotemea uliotelekezwa umekosa wachimbaji wa kuchimba madini yaliyopo,narudia tena Logo pekee ya simba ikitumika vizuri kwa mwaka inaingiza zaidi ya hizo pesa,tamasha la Simba day likiandaliwa vizuri linaweza kuingiza si chini ya 2 bilioni kwa kila mwaka,bado ada za wanachama ,vitega uchumi ikiwemo majengo yale mawili yote kwa thamani huenda yakaifka zaidi ya bilion za pesa ,Simba inautajiri ambao umeshindwa kuinuifaisha yenyewe,leo hii ukisema uje kwenye upande wa hizo hisa kulingana na thamani ya simba pengine hisa moja ya simba ingeweza kuuzwa si chini ya tsh 10000 kwa kila hisa.
Sawa anainunua kwa mtindo wa hisa je ni sahihi yeye kujipangia bei? hapa ndio panadhihirisha kuwa Simba na wanasimba wake NI SAWA na ule usemi wa penye udhia penyeza rupia?
Kwa nini Simba wasingepanga bei wao wenyewe,au wakatangaza kuuza hisa kisha hao matajiri wakajitokeza kununua?
Mwisho wa siku Simba itabaki kuwa ni ya wanasimba ,kama ni hivyo je siku ikitokea Mo akaamua kuuza hisa zake zote kwa tajiri mwingine ambaye haifahamu Simba na hana mapenzi ya kweli na Simba unadhani kuna ambacho kitafanyika?