mh, Rais atakuwa hajafuta hasa sikukuu ya Uhuru. Alichofanya ni kuja na style mpya ya kuadhimisha walau kwa mwaka huu. kaongea juu ya watu kufanya usafi Siku hiyo. sijui mwakani atarudisha utaratibu wa kawaida au la! .Hill namwachia mwenyewe. Binafsi kinachoudhi hasa ni Siku hiyo kuisha kwa gwaride tu. Inashangaza siku muhimu namna hiyo, hakuna hotuba yoyote inayotolewa kama ukumbusho (reminder) kwa watanganyika juu ya Uhuru wao na hata kukazia values zinazoendana na Uhuru wenyewe. sioni kabisa mantic ya kutazama gwaride tu na kukosa nafasi ya kuwahasisha watu (to inspire them) kuhusu maana ya Uhuru na kujua maana yake nini walau kuwajenga wale ambao hawakuwepo wakati huo na hata waliokuwepo kukumbusha context ya Uhuru ukilinganisha na sasa. wakati Rais atakapofikiria kuadhimisha siku hii mwakani asisahau kuimpose suala la hotuba. it is an important part we miss in terms of celebrating uhuru.