Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,866
- 4,252
Wanaotuambia tunawajua
Tunaoambiwa tunajulikana
Wameshatuona tumelala sana
Yani tumelala hadi tunakereketa
Wamechezea sharubu hadi tumezoea
sasa wameamua kuchezea kende na tunaelekea kuzoea
Wanaanza kuchezea mifumo ya taka na hii ni kutuamsha tu
Kweli tunaruhusu mifumo hiyo kuchezewa?
Wanakasirika ni kwa nini hatushituki
Wakati fulani mama alinipiga kwa kuwa nilikuwa mwoga
Basi tuwaache wenye uthubutu na wateule waendelee
Tuendelee kucheza na keyboar nao wakichezea mifumo yetu ya taka
Keyboard warriors vs asshole warriors
Uwiano wa dola na raia
Ni sawa na uwiano wa punje ya hindi na mhindi
Dola ni raia. Nao wana hisia na utambuzi
Watawala ni watumishi wanaotumikiwa na kuabudiwa
Mjeledi mmoja utaangamiza kijiji? kwa hofu yetu itawezekana
Anayetusemea anasemwa, anatukanwa, anadhalilika.
Ni nje na ndani ya viunga vya mahakama na jela
Vitendea kazi hivi vilivyokuwa kimbilio la wenye haki
Wahuni wamevipakata na wanavitomasa. Havisemi
Tunaulizwa nguvu zetu zipo wapi?
Kichwani? Kinywani? kwenye misuli? Ni Mapafu ya kukimbia?
Hofu. Tumsifu anayetengeneza hofu
Maana tumeshindwa kuikabili kwa kuiamini
Tumeikumbatia kwa kuhisi maumivu kabla ya kipigo
Wakati mwingine tunaamini hatuwezi kwa kuwa hatujajaribu
Mara hadi Mtwara. Kigoma hadi Dar es salaam
Sasa nimetambua nguvu yetu ni hofu
Tuna nguvu ya hofu. Hofu ya kupoteza
Hofu ya kuwa punje ya ngano. Mpanzi ni hatma yetu
Tuvumilie udhalimu kwa kuwa nguvu ya hofu imetuzidia
Yoshua wetu yupo nyuma ya nondo
mchungaji aliyepigwa na kondoo kutawanyika
Mungu wetu ni mkubwa. Yu hai na ni kimbilio
Yeye tumemtwisha hofu zetu. Yeye atatuamulia
Atatuamulia kupitia sisi wenyewe. Kumbe kuna kimbilio
Tusiache kuliombea Taifa hili. Tusiache kuwaombea viongozi wetu
Wanaotutia hasira waendelee.
Pengine kuna sehemu watagusa, nasi tutaona sasa imetosha.