kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,083
Sina uhakika kama wakuu wanaliona hili, lakini ni ukweli ulio wazi kwamba CHADEMA kinakabiliwa na ombwe kubwa la kiuongozi ndani ya bunge na nje ya bunge.
Sitaki kuamini kwamba Dr. Sla na Zitto Kabwe ndio walikuwa nguzo kuu ya chama hicho, lakini ukweli ulio wazi kuwa tangu tangu kuondoka kwa viongozi hao wawili wajiondoe ndani ya CDM chama hicho kipwaya kote.
Huku nje ni kama hakipo, ndani ya bunge mchango wake ni ziro.
CHADEMA imeongeza idadi ya sura bungeni, lakini hakuna hata mbunge mmoja anayeonekana kuwa na uwezo wa kujenga hoja bungeni kama walivyokuwa Zitto na Dr. Slaa.
CHADEMA ina serikali kivuli bungeni, lakini kama serikali hiyo kivuli haipo bungeni lakini pia hakuna hata mwanasiasa anayeonekana kuwa na uwezo wa kujenga hoja kama ilivyokuwa enzi za Dr. Slaa.
Serikali kivuli ni kama haipo kwasababu mawaziri wake ni kukosa uwezo na weledi wa kujenga hoja pamoja na kukusanya taarifa mbalimbali zinazoweza kuitwa taarifa mbadala za baraza la mawaziri kivuli wa kambi ya upinzani.
Mfano ni bunge letu linaloendelea tangu april mwaka huu, hadi sasa hakuna hotuba hata moja ya waziri kivuli ambayo imeleta msisimko wowote ndani na nje ya bunge.
Hotuba zote walizotoa ni za kuokoteza matukio ya nyuma, bila kutoa mwelekeo ~way forward~ wa wapi tunapaswa kuelekea kama taifa hata wizara za kisekta.
Kinachosikika kutoka CHADEMA hadi sasa ni Ecrow, uuzwaji wa nyumba za serikali, urushwaji wa bunge live na Lugumi, cha ajabu hayang'aniwi mbunge mmoja mmoja isipokuwa kila anayepata nafasi ni hayo hayo tu.
Labda nitoe mfańo mmoja uzwaji wa nyumba za serikali kwa ujumla vinasimamiwa na wizara ya ujenzi na uchukuzi na mawasiliano. Sasa lema anapolizungumzia kama msemaji mkuu katika hilo wakati yeye waziri kivuli mambo ya ndani ya nchi wapi na wapi? Kwanini asiachiwe waziri kivule mwenye dhamana na suala hilo?
Je serikali kivuli bungeni chini ya mbowe haina utaratibu wa kukutana kwanza na waziri kivuli anayehusika na kila wizara kabla ya hotuba yake kuwasilisha na kuifanyia maboresho na kuiongezea nyama na mawazo.
Ifikie hatua wapinzani wabadilike ili wanaonekana wana tija ya kuwepo bungeni kuliko ilivyo hivi sasa ambapo hatuoni hoja zenye mashiko zenye way forwad badala ya kung'ang'ania matukio tu.
Na kama wataendelea na siasa za matukio zilizokosa umakini wasitegemee kuitoa CCM kwa siasa nyepesi wanazofanya.