Ni ipi mipango ya serikali katika kuimarisha benki ya Posta nchini?

Mwabhleja

JF-Expert Member
Jan 27, 2016
1,351
2,058
Katika historia aliyepata kuwa Rais wa Marekani kipindi ambapo kulikuwa na mdororo wa kiuchumi duniani (great economic depression), Franklin Delano Roosevelt aliwahi kuyafunga mabenki kupisha uchunguzi kutokana na kile kilichoonekana kama mchezo mchafu wa kifedha ambao ulikuwa ukipelekea kushuka kwa thamani ya dola na kutekelezwa dumping strategies ambazo zilikuwa haziendani na hali halisi ya wazalishaji.

Leo hii mimi ningekuwa na mamlaka ningeifungia mitandao ya simu katika kufanya miamala ya kifedha mpaka pale ambapo ningejiridhisha kwamba kodi stahiki inatolewa na makampuni ya simu kwa kufunga vifaa vya kisasa vyenye kutoa taarifa kamili ya miamala.

Nasema hayo, kwa kumulika mwenendo wa benki ya Posta Tanzania kwa maana sioni kama malengo ya serikali ya kuhakikisha benki hiyo inashuka mpaka mashinani kuwahudumia wananchi wa hali ya chini yanatekelezeka.

Kwanza matawi mengi ya benki hiyo bado yapo katika muundo wa kupokea na kutuma barua kuliko kufanya biashara ya fedha (banking). Kuna matawi mengine utakuta watumishi wengi elimu zao hazifanani na shughuli wanazokabidhiwa kwa maana ya ujuzi, maarifa, ubunifu na weledi.

Kuna tawi moja lipo kanda ya ziwa, mtumishi mwenye degree ni mmoja tu ambaye ndiye meneja lakini wengine sijui darasa la saba la zamani, certificate n.k, sasa serikali ina mpango gani na benki ya posta au inajiandaa kuibinafsisha?Serikali ina njia nyingi za kuhakikisha hela inazunguka katika minyororo yake lakini inashindwa kufanya hivyo kwasababu nchi haijulikani inaendeshwa kwa falsafa gani.

Mara ubepari, mara ujamaa, mara mchanganyiko na matokeo yake ni kufanya uwekezaji kama wa ATCL na kufirisika baada ya muda mfupi.Leo nataka kujua, serikali ya Mhe. Magufuli ina mpango gani ya Tanzania Postal Bank (TPB) na pia kama zile milioni 50 kila kijiji zipo basi ningependa kujua ikiwa benki hiyo itatumika kwa namna moja au nyingine tofauti na yalivyopotea mamilioni ya J.K

MWENYE WAZO, FUNUNU, HOJA NA MAONI JUU YA TPB ANAKARIBISHWA HAPA!o_Oo_Oo_O
 
Back
Top Bottom