Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Ilikuwa inakera sana siku za nyuma kumuona amiri jeshi mkuu akiongea kwa kulalamika kama raia ambaye hana mamlaka yoyote yale. Waziri analalamika, mkuu wa wilaya analalamika, waziri mkuu analalamika, raia wa kawaida analalamika, yaani kila mwenye mamlaka alikuwa mlalamikaji.
Awamu ya tano imekuja kivingine, heshima ya vyeo inarudi kama enzi zile za awamu ya kwanza. Badala ya kulalamika na kuongea kama wapenda majungu, tunawasikia viongozi wakitoa maagizo mazito yanayoambatana na ufuatiliaji wa kile kilichoagizwa kifanyike.
Hivi ndivyo Tanzania inavyopaswa kuendeshwa, kile mwenye kuheshimiwa na aheshimiwe, lakini heshima atakayopewa iendane na nia ya kutaka kuzitatua kero nyingi za wananchi. Transparency (uwazi) ni sehemu muhimu sana ya dhana nzima ya hapa kazi tu. Utafanyaje kazi bila ya uwepo wa uwazi. Urasimu na uzikwe rasmi, njoo kesho na ife kifo cha kawaida. Hakuna tena muda wa mijadala na ubishi unaoelekezwa kwa amri halali za viongozi. Hakuna nchi inayoweza kuendelea kama watu wake wanaishia kubakia kwenye mijadala ya kujadiliana mambo mepesi ya juu juu tu.