Chikumba one
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 1,009
- 1,642
Nimekuwa najiuliza kila kukicha sipati majibu, hii Nchi imeishiwaje hekima kiasi hiki, tena kwa muda mfupi tu. Sielewi nini kimetokea. Mtu aliyediriki kumpiga Waziri Mkuu mstaafu, Kiongozi mwenye heshima ndani na nje ya Tanzania, anawezaje kuwa Mkuu wa Wilaya na sasa Mkuu wa Mkoa?
Hivi wakati wa Mwalimu Nyerere huyu kijana angekuwa wapi leo? Kama
Taifa tumejikwaa wapi? Unawezaje kuwa na Nchi ya maendeleo kwa kuwatumia Viongozi wa aina hii?
Viongozi wasiokuwa na maadili ya kazi na kitabia kamwe hawawezi kuwa na matokeo mazuri ktk utendaji wao wa kazi! Viongozi wenye chuki dhidi ya wenzao kamwe hawawezi kulisaidia Taifa. Viongozi wachonganishi, wadhalilishaji, wapenda anasa, wataka sifa tena kwa mambo ya kijinga hawawezi kulisaidia Taifa.
Tanzania ya akina Mzee Warioba, Salim, Malecela, Mwinyi, Bomani, Msuya, Kikwete, Mkapa, Sumayi, Lowasa, na wengineo imetowekea wapi?