Kuna nguvu katika mazungumzo, ikumbukwe kuwa:
[emoji3578] Mnara wa babeli ulistishwa kisa kukosa kuelewana katika mawasiliano
[emoji3578] Ulimwengu uliumbwa katika mawasiliano
Hivyo maisha ya kibubu-bubu uharibu, jitoe sana kwa muda wa kutosha ili kujenga mawasiliano.
Huwezi kuwa na mahusiano au ndoa iliyo imara kama hutoi muda wa kutosha katika Mahusiano hayo
Ni sawa na uwe na bustani na hauipi muda,Lazima itakufa tu
Sababu itahitaji muda kupalilia ,kumwagilia ,kuweka mbolea mpaka ufikie kuvuna
Kama hutotoa muda katika hatua zote kuanzia upandaji wa mbegu mpaka kwenye mavuno tambua kuwa unaweza usipate mavuno kabisa au ukapata kidogo
Ili mahusiano yako yaweze kuwa imara unapaswa kutoa muda wa kutosha kwa ajili ya mwenzako
Mnapaswa kupata muda wa kuwa pamoja nyie wawili wa kuzungumza
Yapo mambo mengi ya kupanga kama mipango katika maisha yenu tarajiwa au kama ni kwenye ndoa mnapata muda wa kupanga mipango ya maisha yenu pamoja
Kupata muda wa kuomba pamoja na mambo mengine mengi cha msingi yampe Mungu utukufu katika majira sahihi
Nimegundua mahusiano mengi hawana muda wa kuzungumza mambo ya maisha yao tarajiwa kwa pamoja sababu wanaishi tu kwenye mahusiano ambayo hayana malengo yoyote
Nyie mliopo kwenye mahusiano wekeni malengo yenu mbalimbali na myasimamie malengo yenu makubwa yawe ya kuimarisha katika maisha ya kumjua Mungu zaidi na kusaidia katika mambo ya kila siku
Udhaifu wa mwenzako msaidie aweze kushinda
Huwezi kufahamu haya yote kama hutakuwa na muda wa kutosha wa kumfahamu mtu uliyenaye
Mwenzako ni mdhaifu katika kutunza pesa hakikisha unamsaidia anakuwa mtunzaji mzuri
Mwenzako ni mvivu katika kusoma neno ,maombi ,kusoma vitabu na mambo mengine mzuri msaidie na mfundishe
Wekeza muda wako kwa yule umpendaye
Msaidie na yeye awe imara na yote haya ni nguvu ya mawasiliano
AsanteNashukuru kwa muda wako
[emoji3478] Na Mjenzi Ally Baudouin
Mwalimu wa Kizazi Kipya Cha Kristo
_____________________________________
View attachment 2322861