Nguvu inayotumika kuzima upinzani ni kubwa

Papa1

JF-Expert Member
Apr 21, 2012
2,017
2,210
Rais wangu JPM, naamini unaamini katika demokrasia, na ndio maana kila mara umesikika ukisema utawala wako hauna itikadi, si wakibaguzi, hakuna CCM wala CHADEMA.

Hata hivyo sura inayoonekana bungeni ni tofauti kabisa na hayo unayotuaminisha. Kwanza umetuondolea Bunge live kwa visingizio lukuki visivyo na mashiko. Pili Wabunge wa upinzani ambao ni wawakilishi wetu umewaminya kupitia mtu wako AT Naibu Spika anatumia kila mbinu kuwanyima fursa ya kutoa maoni na hoja tulizowatuma. Sasa mnatafuta mbinu ya kuwazuia wasiongee nasi katika majimbo. Napenda kujua shida yako hasa ninini? Hutaki upinzani? au hutaki kukosolewa? au hutaki kushauriwa? au hutaki vyama vingi? au hutaki maoni mbadala?

Tafadhali Mheshimiwa, toa yaliyo moyoni mwako ili tuelewa unakotupeleka ili tutembee wenyewe kuliko kutuburuza. Tukikuelewa tutakwenda tu, na hata uchaguzi wa 2020 twaweza kukuachia tu kama alivyoachiwa Dr. Shein huko Zanzibar. Kuwa muwazi, Tanzania inawatu wenye akili tutakuelewa tu!
 
OMS.
One Man Show.
Haambiwi, Hakosolewi, Hasikilizi, Hafundishwi, Haelekezwi ,Hutaki hivyo vitu.
 
Tena hwshauriki; na mimi nilitarajia kuwa angekuwa hiyo ila kimsingi ameyapita Matarajio yangu hasa anapoonekana kufanya kazi ya mawaziri na kupoteza haiba ya uraisi; anashangaa shangaa madudu ya awamu zilizopita kama kwamba yeye hakuwahi kuwakwenye baraza la mawaziri.
Tulimtaka dictator na tumempata. tumvumilie hata lini?
 
Back
Top Bottom