Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,208
- 4,406
NGURUWE NA PUNDA.
1)Ana sura ya huruma,na akili za kichwani.
Ye mjanja kama kima,ila muwizi jangwani.
Nembo yake kama puma,mruka porini shimoni.
Nguruwe mteke punda,umbebeshe mizigo.
2)hawezi rusha mateke,mshamba tangu zamani.
Mzembe ila makeke,awaziaga tumboni.
Hadi leo ni mpweke,japo shibe i shambani.
Nguruwe mteke punda,umbebeshe mizigo.
3)kwake ni domoghasia,maisha yake jeshini.
Mandamano achukia,ajua chake kiini.
Watu wakikisikia,atafukuzwa zizini.
Nguruwe mteke punda,umbebeshe mizigo.
4)adanganyika na pipi,na kutoa vya shambani.
Hata umseme vipi,hakingii akilini.
Vipi tuwambie yapi,yawakae ubongoni.
Nguruwe mteke punda,umbebeshe mizigo.
5)awafungapo midomo,tutasema mikononi.
Domo likiwa kikomo,tutawaza akilini.
Majuto ndo liwe chumo,tuwatoe mitaani.
Nguruwe mteke punda,umbebeshe mizigo.
Shairi=NGURUWE MTEKE PUNDA.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010150
iddyallyninga@gmail.com