Ngoma ya escrow kumbe ni standard chartered

Hana hoja alafu umetumwa kumtetea huyo prof:? mbona mnapopewa hiyo misaada huwa hamutoi maelezo marefu kiasi hiki, za mwizi arobaini tu endelea kutoa maelezo marefu ila wananchi tuna akili zetu za kuchanganua mambo
 
Blah blah blah unajua ada tunayolipa babro kwa ajili ya watoto wetu?

ada inalipiwa kutokana na uwezo wa mzazi kama Harvard, kama wewe kwenye fomu umetaka misifa ya kuonekana unaingiza hela nyingi shauri lako!
 
Nani kasema Rugemalila kumpa Prof Tibaijuka bilioni 1.6 ni kosa, hakuna. Kinachosemwa hapa ni kwamba pesa aliyopewa Prof Tibaijuka ni ya wizi, ilitoka kwenye akaunti ya Escrow. Unaweza kujiuliza Prof angejuaje: utetezi dhaifu sana. Kupokea mali au pesa ya wizi ni kosa na ndiyo sababu kutokana na kiwango cha fedha hiyo kuwa kikubwa wenye akili tunaamini Prof alijua huu ni mgawo wa shukrani.
Umejipinda sana kutetea wizi huu, mara nyingine ujumbe kama huu waandikie wajinga wenzio.
 

Inawezekanaje PAP kuilipa VIP $75,000,000 + $7,000,0000 za kufuta kesi kwa 30% shares iliyokuwa nazo IPTL, halafu kuilipa PiperLink (kampuni feki)/Mechmar only $3000 kwa 70% shares za hiyohiyo IPTL? Huyo JMali aidha ni James Rugemalira au Jerome Rugemalira
 
Haya sasa kumbe waliopokea hela hawana makosa na tatizo imekuwa hela yenyewe ni chafu tu. Ina maana hakuna aliefisadi moja kwa moja au mbona amtueleweshi vizuri sisi raia?

Kwanza madai yenyewe mapya ya kukokotoa upya capacity charge hayakuamuliwa na mahakama zetu na yamekuja baadae sana wakati watu wameshalipwa kama mahakama ya Tanzania ilivyoagiza. Mahakama ya uingereza ndio iliotoa shauri la kukotoa upya capacity charge (huko ni kama kuongeza chumvi kwenye ugomvi wa IPTL na Tanesco) na kumrudisha standard charter kwa nguvu za kikoloni.

Na hao wadai wa standard charter walipoitwa na jaji utumwa kuja kutetea madai yao hawakutokea wakitegemea mahakama ya uingiereza itoe maamuzi ya kuwa favor wao, baada ya kuona Tanzania ina jurisdiction power to decide on the matter ndio wanaomba kesi isimamishwe, isitoshe wao si wabia bali ni wadeni wa mmbia kwanini wanatafuta remedy ya fidia na habari za Tanesco kunufaika na mitambo wakati wabia walikuwa na mzozo na umeme unahitajika. Standard charter walitakiwa wa deal na Rugemalira kwanza kuhusu deni lao aliloacha mechamar lakini tamaa na wao ndio wakaona wanaweza fanya forceful take over; tangia lini benki ikafanya biashara ya umeme.

Ni mwehu tu anaeweza watetea standard charter si ajabu jaji akaona PAP achukue IPTL hawalipe tu hela yao hao standar charter that is what they deserve and nothing more wapuuzi wakubwa wanadhani bado sisi koloni lao.

Isitoshe hawana hata hizo hati za shares wanazodai wamezirithi evidence tu ya kuwa mechamar alikopa na aliacha hisa benki ambazo wanadai wamerithi.

Watanzani tuamke na tuache kutumiwa na mafisadi unaweza ukawa na harisa sana na Ruge kwa matendo yake ya awali kwenye swala la IPTL in the 90's lakini yote ni matokeo ya serikari weak.

Hila hili la sasa la mafisadi kutaka kulipeleka shirika kwa wazungu by force hapana kwakweli, kwanza ni kamati ya PAC kupitia huyuhuyu zito ndio wanaofanya PAP apate shirika kwa sababu ni wao waliotoa mwongozo wa kisheria Tanesco isimiliki mitambo ya IPTL in any circumstances si ndio maana leo kampuni lina amia kwa matapeli. Who knows kwanini zito alishauri hivyo huko nyuma huyu chalii ni mchumia ata mimi naanza kumuona for what he is anatumika tu kama mpira wa kitandani hana tofauti na Andrew Chenge binafsi ni mtu pekee ambae ningependa kuona hili la escrow linamtoa kwenye siasa kabisa i have had enough of this old reprobate kama kweli kapata 1.6 bn; he has played a big role to hinder our economic development kila sehemu aliyoshiriki.
 
Rugemalira alianza kuzi value shares zake na kutaka kuziuza since 2002 at $100 mil. Isipokuwa mgogoro tu wa ubia ukawa tatizo ndio maana akauza kwanza ili PAP amalizane na wabia kumbuka kulikuwa na wind up mahakamani aliyofungua VIP kuna mengi hapa lakini siwezi kuwa upande wa standard charter hata kama Ruge nae ni shetani kwa upande wake, be it within the law akishirikiana na wahuni wengine kufanikisha uhuni wake.
 

kwani rugemalira ni mlalahoi mpaka ashukiwe namna hiyo? ungekuwa wewe ndio umetoa msaada wa bilioni tungeshangaa, rugemalira ana hela toka enzi hizo anamiliki tritel, misaada ya mamilioni kwake kawaida tu. Hivi leo ikigundulika Mengi hajalipa kodi utadai na fedha alizotoa kwa tibaijuka mil 250 kwenye shule ile ile nazo ni za wizi?
Pili, Rugemalira ameuza hisa zake kwa sethi, kama sethi aliiba hakuna tatizo, fedha zitarudishwa na rugemalira atarudishiwa hisa zake 30% kama zamani. Kuna tatizo hapo?
 

sasa hilo swali anatakiwa kuulizwa nani rugemalira ambaye kalipwa kiwango stahiki kwa hisa zake na KALIPA KODI, au TRA na Sethi? Kwa nini mnamzonga rugemalira wa 30% halali badala ya aliyeuza na kununua 70% kifisadi? kama mimi ni rugemalira mmojawapo basi naomba kwa heshima na taadhima nikuite Reginald mengi!
 
Kitu nachokiwaza sana ni kwanini ile share ya 70% ya Singasinga haiongelewi kabisa badala yake tuko busy na 30% ya VIP Eng.? Hapa panahitaji umakini angalieni tusiwe tunalishwa matangopori na ku-uacha ukweli wote pembeni.

Hii hela ya Singasinga wamekula akina nani?
 

Zote ni pesa haramu zilizopatikana kwa njia ya kitapeli na rushwa. Nani kalipwa kiasi gani na nani that's irrelevant.
 

No simple answers to complex legal issues like this. Halafu kuna tofauti kati ya kudai kuwa na 30% shares kwenye IPTL (issue ambayo ilikuwa mahakamani kwani $13.5 million ambazo VIP inadai ililipa kwa 30% shares hazikuwa registered na Mechmar. Uhalali wa 30% shares za VIP kwenye IPTL was in dispute), na kulipwa pesa haramu zilizotokana na grand corruption na utapeli uliotukuka. Kama Rugemalira kalipia kodi au kagawa zote it still doesn't change the facts kwamba kalipwa pesa haramu, na alifahamu dili nzima.
 
ada inalipiwa kutokana na uwezo wa mzazi kama Harvard, kama wewe kwenye fomu umetaka misifa ya kuonekana unaingiza hela nyingi shauri lako!
jMali jMali sasa unapotoka
au umevuta kwa Ruge?
maana toka majuzi ww ni kutetea huo wizi mpaka tukakushangaa
Pinda ametakiwa ajiuzulu na hapo ndipo Baba yako Rugemalila atakapozirudisha na hela zetu zote alizowagawia


 
Last edited by a moderator:
jMali jMali sasa unapotoka
au umevuta kwa Ruge?
maana toka majuzi ww ni kutetea huo wizi mpaka tukakushangaa
Pinda ametakiwa ajiuzulu na hapo ndipo Baba yako Rugemalila atakapozirudisha na hela zetu zote alizowagawia


sijatetea wizi wa pesa za umma, nimemtetea james rugemalira, kuna tofauti hapo. Elewa kuwa James rugemalira akirudisha pesa na yeye hapo hapo atarudishiwa umiliki wa IPTL kwa asilimia 30! Kuna wizi gani hapo?
 

FACT: hizo 30% ambazo wewe unadai was in dispute, ndizo zilizomuwezesha Ruge kuiweka IPTL mufilisi under RITA kupitia mahakama. Kama ingekuwa hazitambuliki hilo liliwezekanaje?
Pili, kutokana na ripoti ya PAC, ruge alitambulishwa kwa sethi na prof Mhongo, ruge alilipwa "chake" (maneno ya zitto), sasa hapo alifahamu vipi dili?
 
Tanesco imeshtakiwa kwa kuwa ni mdhamini wa IPTL wakati IPTL inakopa ilipeleka barua zinazoonesha kuwa inalipwa pesa na Tanesco. Na tanesco ikaridhia
Na wakati wa mauzo Standard Charterd Bank iliweka zuio likatupwa na mahatma a zetu za kifisadi sasa wafanyaje wakaenda kufungua shauri kwenye mahakama zinazotenda haki na ninawahakikishia wana jamii tanesco itashindwa na italipa tutaona

Kuhusu mama Tiba umemtetea sana inawezekana alikuja hajui, lakini kutokujua sio kinga ya kuhusika, mfano ukikutwa na ngozi ya ngombe aliyeibiwa nawe ni muhusika Hata kama wewe ulipewa ngozi tu

Kimsingi nionavyo tanesco kama tanesco haina shida, tatizo limo kwa wanasiasa wanaoingilia utendaji wa tanesco, kama mawaziri, makatibu wakuu.

Hakuna kitu kibaya kama gari kukosa dereva Tanzania sasa haina kiongozi mkuu, kila mtu anajiamulia atakavyo wakes hakuna hapo juu yuko zuzu hivyo wanafanya watakavyo.

Haingii akilini mambo kama haya yanatendeka Rais yuko lakini yuko kimya hii ni hatari sana
 
Inashangaza sana hawa waliogawiwa kwa malboro pale mkombozi jinsi wanavyotapatapa. Yaani CAG anasema ni fedha ya umma na pia takukuru inasema ni fedha ya umma pia TRA. Bado jinga linakuja kubishana hapa. Unafaa kutemewa mate usoni!! Na kama ni za bank hao maccm na maasikofu waliozila nao ni wamiliki wa hiyo bank unayotaja? Acha ujinga we ni mtu mzima!!
 
sijatetea wizi wa pesa za umma, nimemtetea james rugemalira, kuna tofauti hapo. Elewa kuwa James rugemalira akirudisha pesa na yeye hapo
hapo atarudishiwa umiliki wa IPTL kwa asilimia 30! Kuna wizi gani hapo?

Kamati imeshapendekeza IPTL itaifishwe na kuwa Mali ua Umma na mm nashauri huyu Nshomile afilisiwe na kufungwa na hata hao ndugu waliopewa gawio hata humu JF watafutwe

cc

MANKA MUSA pendolyimo optimus prime Apollo 11 shadow recruit assanal pitapiti

 
sina tusi la kukutukana matusi yote ya zamani ngoja nitafute jipya ahahahah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…