Kila kukicha watu wanagundua mbinu mpya za kujipatia vitu vya bure. Kuna watu wanatarget watu wenye magari ambao wanahisi wanaweza wakawa na vitu vya thamani. Wengine wanayo magari mazuri amabayo hata huwezi kuhisi, ambayo wanatumia kufuata gari lako mara wakikuona unatoka mahali kama bemnki au wakihisi kuwa una vitu vya thamani kwenye gari lako. Wanakusubiri hadi kwenye foleni, wanagonga gari yako kwa nyuma. Kwa kawaida, katika hali ya namna hiyo watu hutoa lock ya milango na kufugua mlango kuangalia. Wakati huo wewe unapotoka, mtu mwingine anafungua milango ya upande wa pili na kuchukua vitu vilivyoko mbele na kiti cha nyuma. Baadaye wanakuwambia kwa vile wamekugusa tu basi muelewane au wakupeleke mahali mkanyooshe. Unapoingia kwenye gari wao wanakuacha! Kuna bwana mmoja alitoka kuchukua fedha tawi la Kichwele wakamfanyia mchezo huu wakaondoka na 20 million!!Ni muhimu kuchukua tahadhari. usiweke vitu vya thamani kwenye viti, au usiviweke kiasi kwamba watu wanajua ni kitu kama laptop au briefcase. Unapoendesha hakikisha milango ya gari lako imefungwa. Kama utagongwa kwa nyuma au hata mbele au pembeni usiharakishe kutoka kwenye gari.