Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ambaye yuko ziarani katika nchi za Afrika, leo hii ataizuru Rwanda, ambako anatarajiwa kutembelea kituo cha makumbusho ya mauaji ya kimbari mjini Kigali. Akizungumza jana mjini Nairobi, Kenya, Netanyahu alisema Afrika haina rafiki bora zaidi ya Israel katika masuala ya usalama na maendeleo.
Netanyahu ni waziri mkuu wa kwanza wa Israel kufanya ziara katika mataifa ya Afrika Kusini ya Jangwa la Sahara katika muda wa miongo mitatu. Akiwa nchini Kenya, Netanyahu alifanya mazungumzo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta juu ya ushirikiano katika kupambana na ugaidi, na katika sekta za nishati na kilimo.
Israel inanuia kuutumia utaalamu wake katika masuala ya usalama na sekta nyingine kuzisaidia nchi za Afrika, kuvutia uungwaji mkono wa nchi hizo katika baraza kuu la umoja wa mataifa, ambako kwa kiwango kikubwa Palestina inatambuliwa kama mwangalizi asiye mwanachama. Ziara ya Netanyahu barani Afrika ilianzia nchini Uganda, na itahitimishwa nchini Ethiopia.
Chanzo: DW