Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,286
- 10,831
Ofisi yake imethibitisha leo kwamba Netanyahu atabaki kuwa waziri mkuu, lakini wizara za afya, maswala ya kijamii, kilimo na inayowashughulikia wanaoishi nje ya nchi hazitakuwa tena chini ya mamlaka yake.
Jakov Litzman, naibu waziri wa afya wa zamani, ameteuliwa kuwa waziri mpya wa afya. Watakaochukua nyadhifa za wizara hizo na ofisi nyinginezo watatangazwa wiki ijayo.
Mwendesha mashtaka mkuu alitangaza mwishoni mwa mwaka jana kwamba Netanyahu atashtakiwa kwa makosa ya kuhusika na hongo, udanganyifu na uvunjaji wa uaminifu.
Chanzo: DW Swahili