Neno Nalo

Neno Nalo

mirymicaiah605

Senior Member
Joined
Apr 6, 2014
Posts
107
Reaction score
17
Ukitaka kujua Uzuri wa Mbinguni waulize MALAIKA....Ukitaka kujua ukali wa moto wa Jehanum muulize SHETANI ila KAMWE USITHUBUTU kuwauliza Wanandoa kuhusu "Habari za Ndoani" Watakwambia Siasa Tupu...Very few talk the truth kuhusu Maisha ya Ndoa ila Wengi ukiwauliza
"Jamani Nioe huko hali ikoje" utawasikia wanakupa majibu Mepesi kama Wabunge wa UKAWA,"aah huku raha bwana,huoni nlivyonenepa,cheki kitambi nang'aa nikirudi nakuta chakula tayari,nalala uchi namega unyumba nnapojisikia"
THUBUTUU!!

Wanakutajia vitu very obvious..Kwani siwezi kulala uchi ghetto kwangu??Siwezi kunenepa mwenyewe nikiamua?HALI HALISI HAWAKWAMBII Hawatakwambia Wiki ya 2 hii "mke kagoma kukanyaga klachi" gia hazipandi unyumba nehi...Hawatakwambia jinsi Mawifi wanavyozingua kisa mwaka wa 2 huu hawajaona mtoto wala dalili za kaka yao kutumwa Udongo...Hawatakwambia

Sleepless nites za magomvi ya meseji walizofuma toka kwa Ma-Ex..Hawatokwambia kwamba Mkewe wala hajisikii tendo la ndoa kama Wiki za mwanzo ila anampa basi tu kutimiza mradi...WALA HAWAKWAMBII Wao ni Ooh huku kutamu sana yaani Bajeti siku hizi anasimamia mke wangu..

WALIOOA/KUOLEWA usiwasikilize sana,wanakusukuma kitonga ukitiririka tu wao wanakucheki,mwisho wa siku wanataka tu uzame ili wote muanze kulia Chorus inayofanana..Yaani wanandoa kama kwaya kuu vile..Wote mnaimba Sauti ya Juu...Mi nawamegea maana nakaa nao..wananiuliza maswali halafu baadae wanajisahau wananisifia,"Bora wewe kaka bado hujaoa aisee Dah"

Ukiingia INGIA TU ila sio kwa sababu Sam kakushauri,hatokwambia yote!
 
watu wengi hawajui kwa nin anaoa/olewa hapa ndo mwanzo wa tatizo, ni kama kupanda basi bila kujua linaishia wapi, utalamika umeshushwa njiani kumbe wenzio wameshafika mwisho wa safari
 
Nidhani mjadala kama huu uliisha baada ya Lara1 na malaika zake kujivua gamba. Kifupi pitia nyuzi za lara1 kuhusu kuita ndoa ni taasisi ya kinafiki...kule majibu yapo mazuri huku itakuwa ni marudio.

Niseme ndoa ni mpango wa Mungu kutunusuru na dhambi rejea amri kumi za Mungu alizokabidhiwa babu yetu Musa. Ukitumia akili zako pekee utaishia kutuonyesha uzoefu hasi katika muungano huu mtakatifu. Jambo la kukumbuka ni kwa kila aina ya maisha utakayo chagua inachangamoto zake, na hazikwepeki.
 
Kwa hiyo unategemea uoe afu usikute changamoto yoyote kwenye ndoa? Nyie mliooana ni malaika au? Kokote tu unapoishi iwe kazini au nyumbani, hujawahi kupishana lugha na mtu? Changamoto lazima ziwepo na zikitumiwa vizuri basi zinaboreshaa ndoa, kwa sababu zinawafanya mjue kwamba mwenzangu hapendi hiki na hiki.

Mnavyozivuka changamoto pamoja ndo mnazidi kuimarisha mahusiano. Afu kila mtu anaitengeneza ndoa anayoitaka, wewe oa au olewa afu utaamua mwenyewe kuitengeneza ndoa yako, either iwe paradiso au jehanamu
 
Back
Top Bottom