Jamani wanaJF,
Naomba mnieleweshe kuhusu hili jina la BONGO. Nimekuwa nalisikia siku nyingi sasa na pengine kuunganishwa na maneno mengine kama BONGO FLAVOR , kwetu BONGO , KI-BONGOBONGO Na kadhalika.
Natanguliza shukrani
kaka hiii nimisimu mfano neno bongo maana yake akili kwa hiyo watu waliona kuwa wakazi wa dar wana uelevu wa mambo mengi hivyo wakaamua kupaita bongo
kaka hiii nimisimu mfano neno bongo maana yake akili kwa hiyo watu waliona kuwa wakazi wa dar wana uelevu wa mambo mengi hivyo wakaamua kupaita bongo
lilitoholewa kutokana na neno ubongo ndipo lakapatikana neno Bongo. Maana yake ili uishi Dar lazima kutumia ubongo (akili) sana tofauti na mikoani. Baadaye maisha ya Watz wote hata wa mikoani yamekuwa magumu hivyo Tz kwa ujumla sasa hivi inaitwa Bongo. l
Ni kabla ya hapo mkuu. Baada ya vita vya Kagera 1978/9 hali ya uchumi ilisambaratika na maisha kuelekea kuwa magumu. Wakati huo Nyerere alituahidi mambo yatanyooka ndani ya kipindi cha miezi 18 na tukatakiwa "tufunge mikanda". Hali ilizidi kuwa mbaya na mwanzoni wa 80´s msemo wa "jua kali" na "bongo" ndipo ulipoanza kushamiri. Yaani jamaa anakuuliza vipi mambo? na wewe unajibu mambo jua kali (yaani ni kusota). Bongo ilitokana na swala la kutumia ubongo ili kusavaiv mjini. Na hapo ndipo Dsm ilipogeuka kuwa bongo. Bongo jua kali. Baadaye na hadi sasa bongo inamaanisha TZ kwa ujumla!Bongo=AKILI...kuishi DSM ilimlazimu/inamlazimu m2 kuishi kiujanjaujanja, ku2100 mbinu mbadala kuendesha maisha ya kila cku. "mission town" lakini baada ya hali ya maisha kuwa ngumu wa2 wote Tz mijini na vijijini, kuanzia mkulima, mfanyakazi na hata mfanyabiashara inambidi kuishi kiujanjaujanja, kutumia bongo kuendesha maisha...neno bongo lilianza kutumika miaka ya 1984. Wakati huo unapanda treni pale moshi saa 10 jioni nakufika bongo saa 4 asbh cku inayofuata!