NEC waanza kufanya tathmini ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 2015.

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
740
485
NEC waanza kufanya tathmini ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 2015.


NEC3.jpg



Tume ya taifa ya uchaguzi nchini (NEC) imeanza zoezi la kufanya tathimini ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana 2015 unaolenga kutambua mafanikio na changamoto zilizojitokeza na kuanza kuzifanyia kazi zoezi litakalofanyika katika kanda zote nchini likiwashirikisha wadau mbali mbali zikiwemo asasi za kiraia.

Anakizungumza kwa niaba ya mwenyekiti wa tume hiyo jaji mstaafu Damiani Lubuva, kamishna wa tume hiyo Prof Amoni Chaligha amesema miongoni mwa mambo yanayofanyika ni pamoja na kuangali mchango wa wadau mbalimbali wakiwemo wananchi katika kushiriki nakufanikiksha uuchaguzi huo ukiwemo uliotolewa na asasi za kiraia zilizokuwa zimepewa jukumu la kutoa elimu ya uraia.

Baadhi ya wawakilishi wa taasisi hizo za kiraia wamesema tatizo la ukosefu wa elimu ya uraia na faida zake bado ni kubwa na wameitaka tume kuhakikisha inakuwa ni agenda ya kitaifa na itolewe wakati wote badala ya kusubiri wakati wa uchaguzi.

Hata hivyo wawakilishi wa baadhi ya makundi likiwemo la walemavu na wazee wamesema bado hawajashirikishwa ipasavyo kutoa mchango wao na wamesema asilimia kubwa ya wazee na walemavu wa kusikia walishindwa kushiriki uchaguzi kutokana na kutowekewa miundombinu ya kuwawezesha kusikiliza sera za wagombea wakiwemo wakalimani.

Source: RadioOneStereo
 
Back
Top Bottom