Mwifwa
JF-Expert Member
- Apr 3, 2017
- 46,921
- 122,189
Vituo vingi vimeandikisha wapiga kura zaidi ya 500, NEC wanasema katika uchaguzi wa mwaka huu kituo kimoja kitahudumia watu wasiozidi 500.
Kwa mantiki hiyo vituo vitakuwa vimegawanywa na majina yatakuwa yamegawanywa na kupelekwa kwenye vituo vipya.
Kwa wale ambao majina yao yamehamishwa kwenye vituo vipya ili kukidhi matakwa ya kituo kimoja kuhudumia watu wasiozidi 500, NEC mnatujulisha vipi vituo vyetu vipya ili kuepuka usumbufu wa Octoba 28, 2020 pindi ambapo kila mmoja wetu atakapoandaa jambia lake maridhawa kwa kazi mahususi ya siku hiyo?
Kwenye kuhakiki taarifa zetu mumetupa namba *152*00# ambayo tunaitumia kupitia simu zetu kujua taarifa zetu.
Kwenye hizo taarifa naombeni muongeze kipengele cha kutujulisha kituo cha kupigia kura endapo jina litakuwa limehamishwa kituo kipya tofauti na kile ulichoandikishwa.