Ndugu yangu!! Kwanini unataka kuniua bure??

ONTARIO

JF-Expert Member
Oct 16, 2013
1,891
2,000
Salute bosses...

Mara ya mwisho kupost hapa MMU ilikua miaka miwili iliyopita, bado nilikua chuo enzi hizo - kukimbizana na totoz, kuvaa macheni n.k, lkn sasa tumekuwa hata vitu vinavyozurura ndani ya kichwa navyo vimebadilika. Mada ya leo nyepesi sana, lakini muhimu mno.

Dini ya Uislam inatufundisha upendo na si chuki... Undugu na si uadui... amani na si vita... ushirikiano na si ubinafsi... umoja na si utengamano.
Sawa na mafundisho ya Ukristo,
Sawa na mafindisho ya Ubuddha,
Sawa na mafundisho ya kimila,
kila sehemu tumasisitiziwa kuhusi nguvu iliyopo katika upendo.

Kwanini ujaze chuki kwenye moyo wako badala ya upendo?!
Jirani yako kafanikiwa kununua gari mpya, ghafla unaanza kumchukia. Unaingia jikoni unaanza kupika majungu, fitna na maneno ya kinafiki. Malipo yake ni nini?! Kwanini usingetumia nguvu hiyo kuungana na jirani yako akupe mbinu mbadala iliyomwezesha yeye kupata hiko kitu.

Staff mwenzio kapandishwa cheo, ama anapendwa zaidi hapo ofisini, wewe unaanza kuleta wivu & hasira, unamchukia mtu ambae hajakukosea jambo. Unatamani hata afukuzwe kazi, kana kwamba huo mshahara wake utakua unalipwa wewe. Kwanini...?! Unaanza kuchocha maneno ya uongo ili staff wengine nao wamchukie. Faida yake ni nini haswa?

Ndugu yako wa karibu kapata mke ama mume mzuri, unaanza kumchukia - bila sababu, bila kosa. Unaanza kumchukia na kuchokonoa ndoa yao, yote ya nini? Mwisho wa hizo unaingiza pesa ngapi kwenye account yako?! Mwanaume unamuonea wivu mwenzio kupata mke makini, ulitaka uolewe wewe?!

Mzee wangu Les Wanyika aliwahi kuimba...

Hasira za nini wee bwana?
Hasira za nini wee bwana?
Wataka kuniua bure baba...
Wataka kuniua bure baba...
Yule si wako nami si wangu, chuki ya nini kati yangu mimi na wewe?
chuki ya nini kati yangu
mimi na wewe?

Chuki ni tabia za kilozi sana. Chuki, wivu na unafiki ni njia rahisi ya kukuletea umasikini, stress na magonjwa mengine ya kienyeji enyeji. Unachelewesha baraka zako kisa mambo kama haya.

1 Wakorintho 13:4-7

4. Mwenye upendo huvumilia, hufadhili; mwenye upendo hana wivu, hajidai, wala hajivuni.
5. Mwenye upendo hakosi adabu, hatafuti faida yake binafsi, wala hana wepesi wa hasira; haweki kumbukumbu ya mabaya
6. hafurahii uovu, bali hufurahia ukweli.
7. Mwenye upendo huvumilia yote, huamini yote, na hustahimili yote.

Love your neighbour as you love yourself. Huu ndio urafiki wa ukweli, ushkaji wa ukweli, swaga za ukweli, undugu wa ukweli, usela wa kijanja, ujamaa wa faida. Hakuna haja ya kumchikia ndugu yako, kwanini unataka afe bila sababu?!

Salute!!
 

The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
14,623
2,000
Shukrani sana ONTARIO , dunia ingekuwa mahali pazuri sana endapo tungeishi kwa ile kanuni ya kifalme inayosema " ...watendeeni wengine kama ambavyo mngependa wao wawatendee ninyi" kwa maana nyingine usimfanyie mwingine kitu usichopenda kufanyiwa wewe.
 

God'sBeliever

JF-Expert Member
Sep 1, 2015
5,828
2,000
Shukrani sana ONTARIO , dunia ingekuwa mahali pazuri sana endapo tungeishi kwa ile kanuni ya kifalme inayosema " ...watendeeni wengine kama ambavyo mngependa wao wawatendee ninyi" kwa maana nyingine usimfanyie mwingine kitu usichopenda kufanyiwa wewe.
Dunia yetu nzur sema binadamu nuksi.
 

BIGstallion

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
6,391
2,000
Mara nying nguzo imara ni kusamee na kuishi ndoto zako,wivu na roho mbaya haijaanza Leo tokea tuko eden,..anyway Mara nyingi ukiona Una karibia mafanikio utapata maadui wengi kuliko marafiki,lakin ukiishi mafanikio yako marafiki watakua wengi zaidi,
 

God'sBeliever

JF-Expert Member
Sep 1, 2015
5,828
2,000
Mara nying nguzo imara ni kusamee na kuishi ndoto zako,wivu na roho mbaya haijaanza Leo tokea tuko eden,..anyway Mara nyingi ukiona Una karibia mafanikio utapata maadui wengi kuliko marafiki,lakin ukiishi mafanikio yako marafiki watakua wengi zaidi,
Ufanyeje ili ukae nao mbali coz kila uendapo wapo!
 

ni ngumu

JF-Expert Member
Sep 25, 2016
3,239
2,000
Staff mwenzio anaponunua gari unachukia sababu ameprove kwamba mimi zezeta...kwamba tunapewa mshahara moja lkn mwenzangu kanunua gari mm ht baiskel sina...lzm nichukie niache nichukie ni haki yangu..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom